Padre Saba afariki akipatiwa matibabu Dar

Wednesday August 04 2021
p[adripiccc
By Happiness Tesha

Kigoma. Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Raymond Saba amefariki duniani Agosti 3, 2021 majira ya saa 1 jioni katika hospitali ya Rabinitsia iliyopo jijini Dar es salaam aliyokuwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa Askofu wa jimbo katoliki Kigoma, Evarist Guzuye, amethibitisha kifo chake, akisema misa takatifu ya mazishi itafanyika katika kanisa la Mtakatifu Marko Kabanga, wilayani Kasulu siku ya jumatatu, Agosti 9, 2021.

Amesema Agasti 7, 2021 siku ya jumamosi, watakuwa na misa takatifu kurasini jijini Dar es salaam, ambapo Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa ajili ya kumwombea na kuuaga mwili.

Advertisement