Padri ajeruhiwa makazi yao yakivamiwa

Thursday September 30 2021
mapadripic
By Bakari Kiango

Dar es Salaam. Watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia makazi ya mapadri wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Bakhita Parokia ya Mtoni Mtongani na kumjeruhi padri mmoja.

Inadaiwa kuwa tukio hilo lililtokea usiku wa kuamkia leo Alhamisi  Septemba 30, 2021  ambapo watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga pamoja na nondo.

Walimpiga nondo ya kichwa, padre Teri Mambwe.

 Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Yuda Thadeus Ruwa’ichi amekiri kutokea tukio hilo.

“Nimepata taarifa lakini siyo kamili kuhusu tukio hilo. Kulikuwa na uvamizi katika Parokia ya Mtoni na kuna mmoja amejeruhiwa sasa anapata matibabu hospitalini,” amesema Askofu Ruwa’ichi.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke , Richard Ngole hakutaka kukubali wala kukataa badala yake alitoe maelekezo atafutwe Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro ambaye naye alipotafutwa simu yake haikupokelewa.

Advertisement


Advertisement