PASS trust, yahimiza uzalishaji unaofuata misingi ya ukuaji wa kijani shirikishi.

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Nehemia James

Muktasari:

  • PASS Trust ya wahakikishia wadau wa kilimo mkoani Katavi fursa mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mikopo itakayo wasaidia kufanya uzalishaji unaofuata misingi ya ukuaji wa kijani shirikishi.

Katavi. Taasisi ya PASS Trust imezungumza na wadau mbalimbali waliopo katika mnyororo wa kilimo mkoani humo, na kuwapatia fursa wakulima kwa kuwahakikishia watapata mikopo kutoka taasisi za fedha, huku wakihimizwa kufanya uzalishaji unaofuata misingi ya ukuaji wa kijani shirikishi.

Akiongea katika kongamano la wadau wa kilimo lililoandaliwa PASS, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Nehemia James, amesema kuwa umuhimu wa PASS Trust unasaidia sana katika suala la kukopa huku ukisaidia Benki kuwa na uamuzi wa kutoa pesa.
“Uwepo wa PASS unasaidia sana taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wakulima kutokana na dhamana zinazotolewa na PASS Trust,”

James ameeleza kwamba dhamana hiyo wakulima wanaweza kuwekeza katika kilimo ambacho kinatunza mazingira, na kinazingatia ukuaji wa kijani shirikishi, pia hii ni fursa kwa wajasiliamali wote.

Kwa upande wake Meneja wa maendeleo biashara wa Pass trust Herman Bashiri yeye amewataka wadau kuchangamkia fursa zilizopo katika kijani shirikishi.
“Pass trust ni taasisi inayowawezesha wajasiriamali wote waliopo katika mnyororo wa kilimo,” amesema

Ameongeza kwamba taasisi yao imeamua kuhamasisha kampeni ya kijani cha maisha ili kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali kuunga juhudi ya serikali pamoja na dunia kwa ujumla katika suala zima la kutunza mazingira hasa katika sehemu ya kilimo.

Naye mmoja wa wadau waliojumuika katika kongamano hilo, Johari Katandi amesema amefarijika kutambua kuna fursa za upatikanaji wa mikopo kwa wakulima wadogo kama wao, na hivyo
“Upatikanaji wa mikopo kwa sisi wakulima wadogo wadogo utanisaidia mimi kulima kilimo cha kisasa kwa kufuata maelekezo ya kitaalamu,”amesema