Polisi, mahabusu wafariki kwa ajali Geita

Muktasari:

  • Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na mahabusu wawili wamepoteza maisha kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Mwanza


Geita. Watu wanne wakiwemo askari polisi wawili na watuhumiwa wawili wamepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa kwa ajali ya gari iliyotokea jana Jumatano jioni Aprili 27, 2022 Kijiji cha Ibanda barabara ya Geita-Mwanza

Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari ya polisi aina ya Toyota Land cruiser kuhama kutoka upande wake na kwenda upande mwingine na kusababisha kugonga lori.

Amesema watuhumiwa hao walikuwa katika gereza la Butimba ambapo walifikishwa katika mahakama ya Kuu Geita na kusomewa mashtaka yao wakiwa njiani kurudi gerezani ndipo ilipotokea ajali hiyo.

Kamanda amewataja waliopoteza maisha kuwa ni namba G 4467D/CPL Mussa, namba G 5702D/CPL Faraji wote askari polisi Mkoa wa Mwanza na washtakiwa Twaha Said na Tesha Murushindi waliokuwa na kesi namba P1 3/2022 kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya ugaidi na mauaji.

Kamanda pia amewataja waliojeruhiwa kuwa ni PF23158A/INSP Baraka Apila, F8361 D/SGT Berison Sanga wote askari wa mkoa wa Mwanza na Maronja Katemi (52) pia amemtaja dereva wa gari, Berison Sanga mfanyakazi wa kampuni ya Nyanza Botling mkazi wa Igoima Mwanza na Paulo Charles mfanyakazi