Puma Energy inavyojipambanua kwa vilainishi bora nchini


Muktasari:

  • Fursa ya ukuaji wa soko la bidhaa za vilainishi unak­abiliana na changamoto ya kuongezeka kwa bidhaa duni na za kughushi za cha­pa maarufu za vilainishi.

Fursa ya ukuaji wa soko la bidhaa za vilainishi unak­abiliana na changamoto ya kuongezeka kwa bidhaa duni na za kughushi za cha­pa maarufu za vilainishi.

Hali halisi iliyopo soko­ni inatoa wito kwa wadau wakuu na Serikali kuamka kutoka usingizini na kuchu­kua hatua sasa kabla hali haijawa mbaya zaidi.

Katika kukabili kadhia hiyo, Kampuni ya Puma Energy Tanzania, inasi­mama kama rafiki sahihi wa kusaidia wateja wanapok­wama kujua zilipo bidhaa za vilainishi halisi na zenye ubora.

Kuingia kwa Puma katika soko la ndani la vilainishi kunafufua matumaini yali­yopotea kutokana na utitiri wa bidhaa za vilainishi za magendo, za kughushi na zile duni.

Ikiwa ni kampuni iliyoji­pambanua katika vilainishi na ikiendesha shughuli zake nchini tangu Septemba 2011, baada ya kuhodhi shughuli za BP, kampuni hiyo inaon­goza katika soko la Tanzania katika bidhaa za vilainishi na mafuta.

Mfanyakazi wa Puma Energy akitoa elimu juu ya matumizi bora ya vilainishi vya Puma kwa dereva wa daladala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kampuni ya Puma Energy imekuwa ikitoa elimu kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuweza kubadilisha vilainishi kila baada ya miezi miwili hadi mitatu kulingana na safari zako.

Kampuni hiyo inajivunia uwezo wake wa kuhifadhi lita milioni 94, na inaende­sha vituo 70 vya mafuta ya petroli kote nchini na kuhu­dumia viwanja vinane vya ndege.

“Shughuli zetu zinalenga katika kuuza vilainishi na bidhaa nyingine za mafuta kwa wateja wakuu katika sekta ya uchimbaji madini na usafirishaji nchini,” anas­ema Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Dominic Dhanah.

Anasema kuwa madini ni sekta muhimu nchini Tan­zania kwa sababu nchi ina rasilimali nyingi za asili yakiwemo madini ya dhaha­bu, almasi, makaa ya mawe, chuma, urani na nikeli.

“Tunatoa huduma za haraka na zenye ufanisi zai­di kwa kampuni za mafuta na gesi zinazofanya kazi nje ya nchi kutoka Tanzania.

Tulipanua sehemu yetu ya soko katika sekta ya usafiri wa anga, hivi sasa tukiuza mafuta ya ndege na avgas katika viwanja vinane vya ndege nchini,” anaongeza Mkurugenzi huyo.

Anasema kuwa vilaini­shi vya Puma vilizalishwa, kuuzwa na kusambazwa katika nchi nyingi za bara la Afrika na Amerika ya Kati na Asia-Pasifiki.

Mfanyakazi wa kampuni ya Puma Energy akitoa elimu kwa fundi garage juu ya matumizi bora ya vilainishi vya Puma. Kampuni ya Puma Energy imekuwa ikitoa elimu kwa wamiliki wa vyombo vya moto kuweza kubadilisha vilainishi kila baada ya miezi miwili hadi mitatu kulingana na safari zako.

“Hapa Puma Energy, tunasukumwa na uzingatiaji ubora. Puma Energy ime­chagua kwenda na vipimo vya juu zaidi vya bidhaa zote za vilainishi na mafuta kwa kutoathiri viwango vya nyongeza vya bidhaa hizo,” Dhanah anaeleza.

Puma inazalisha bidhaa zote kwa kutumia hifadhi ya mafuta ya msingi ya Exxon Mobil. Mifumo, michakato, taratibu na timu ya vilaini­shi maalum ya kampuni yetu huhakikisha kuwa bid­haa zinafuata viwango vya ubora wa juu zaidi.

Pia anabainisha kuwa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu za kampuni hiyo zimeundwa kuhudumia sehemu mbili; kutoa masu­luhisho maalumu ya wateja wanaomiliki vyombo ya moto (magari, malori, na pikipiki). Pia inatoa masu­luhisho ya mahitaji ya viwandani

pamoja na teknolojia yake ya kipekee ulimwenguni, ina manufaa ya kibiashara yanayoweza kupimika kama vile uokoaji wa gharama kubwa.

Soko la vilainishi

Soko la vilainishi nchini Tanzania linajumuisha zaidi viwanda vya magari, viwan­da na madini, huku vile vya magari vikichukua nafasi kubwa, anaongeza.

Anasema kutokana na ukweli kwamba nchi hiyo imezungukwa na nchi tano zisizokuwa na bahari; hivyo, bidhaa za vilainishi vya vyombo vya moto vina soko kubwa zaidi.

Wadau wakuu wa sekta nyingine wanaona kuwa soko la vilainishi nchini liko thabiti na kwamba ushin­dani unaendelea kuongeze­ka hususan katika sekta ya vyombo vya moto.

Ukuaji wa soko la bidhaa za vilainishi linaweza kukua ispokuwa wimbi la bidhaa za kughushi, duni na za magen­do linaharibu taswira nzima ya soko.

Uwekezaji katika usalama unalipa

Anaongeza kuwa uwekez­aji mkubwa wa Puma Energy katika usalama wa uende­shaji unalipa. Mchanganyiko kamili wa ubora na usalama kwenye vilainishi vyetu, una mchango mkubwa katika kuhifadhi wateja na kupata masoko mapya.

Uachaji alama

Dhana anathibitisha kuwa kampuni hiyo inajitahidi kujitangaza kama msamba­zaji wa mafuta anayezinga­tia ubora sokoni na kubeba imani hiyo kutoka kwa wate­ja wake kikamilifu katika shughuli zake kwa kiasi kikubwa.

Matarajio ya baadaye

Kulingana na Mkurugenzi huyo, Puma inalenga kufikia ubora wa usalama wa kiu­tendaji, kuboresha usimam­izi na udhibiti wa mali zilizo­po, kurahisisha gharama na kuboresha pendekezo letu la thamani kwa wateja.

Hata hivyo, kampuni hiyo ya nishati inajiona ikivuka kizingiti cha ufanyaji vizuri sokoni wa bidhaa zake na kuteka mioyo ya wateja wa bidhaa za vilainishi wanao­penda bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.