Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Babu ambana mkandarasi ujenzi wa hospitali

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameagiza  kuharakishwa kwa ujenzi wa majengo saba mapya ya hospitali ya Wilaya ya Same  likiwemo Jengo la mama na mtoto na kwamba ifikapo Februari mwaka huu yawe yamekamilika.

Same. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameagiza  kuharakishwa kwa ujenzi wa majengo saba mapya ya hospitali ya Wilaya ya Same  likiwemo Jengo la mama na mtoto na kwamba ifikapo Februari mwaka huu yawe yamekamilika.

Majengo hayo yanayojengwa katika kijiji cha Kirinjiko wilayani humo yalianza kujengwa Juni mwaka jana na tayari serikali imetoa zaidi ya Sh2 bilioni.

Babu ametoa maagizo hayo leo Jumapili Januari 29, 2023  alipotembelea eneo linapojengwa hospitali hiyo,  ‘’niwapongeze kwa kazi nzuri na usimamizi mzuri, ninachotaka muongeze kasi kwenye haya majengo, nikija mwezi Februari hayajamalizika sijui itakavyokuwa ila tuongeze kasi kwenye haya majengo, nataka wananchi wapate huduma za afya kwa karibu na kwa urahisi."

"Sioni sababu ya haya majengo kucheleweshwa maana serikali imeshatoa fedha zote, tunataka watu wapate huduma za afya kwa karibu na kwa urahisi, nataka mwakani hospitali hii iwe imeshaanza kufanya kazi."

Amesema azma ya serikali ni kuona wananchi wanapata huduma kwa karibu na kuepuka kutembea umbali mrefu  kusaka huduma za afya.

Awali akitoa taarifa kwa mkuu huyo wa mkoa mganga mfawidhi wa hospitali ya Same ambaye ni msimamizi wa ujenzi huo, Dk Ibrahim Sembua amesema tayari serikali imetoa zaidi ya Sh2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo mapya huku akiahidi kuwa hadi Februari utakuwa umekamilika.