Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Kilimanjaro atoa neno kwa wanaume

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akifurahia jambo na watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Tuleeni, kilichopo kata ya Uru Kusini, wilaya ya Moshi.Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuacha kulea watoto wao pindi wanapozaliwa waache tabia hiyo.

Moshi. Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amewataka wanaume wanaowapa ujauzito wanawake na kuacha kulea watoto wao pindi wanapozaliwa waache tabia hiyo.

Amesema ni jukumu la wazazi wa pande zote mbili kulea watoto wanapozaliwa na siyo kuwatelekeza.

Babu aliyasema hay oleo Desemba 27, 2022 alipotembelea na kutoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika kituo cha Tuleeni kilichopo katika kata ya Uru Kusini, wilayani Moshi.

“Watoto hawa ni wetu na sisi wazazi baba na mama ndio tunaozaa hawa watoto, kwa hiyo una wajibu mkubwa wa kumlea mtoto sasa wewe ukishazaa unatelekeza mtoto alelewe na nani.

“Nitoe wito kama unaona huwezi kumlea mtoto usiende kutafuta mwanamke ukazaa naye, kama unaona huna uwezo au mapenzi na mtoto, humjui Mungu usiende kumtafuta mwanamke umpe mimba alafu umtelekeze,” amesema.

“Hizo tabia tuache, hazina maana na sio ustaarabu wa Watanzania, mapenzi ya mtoto yapo kwa baba na mama,” amesema Babu.

Akizungumzia kituo hicho, mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha Tuleeni, Flaria Faraji amesema hadi sasa kituo hicho kimenufaisha zaidi ya watoto 600 ambao baadhi yao kwa sasa ni madaktari, walimu, wanasheria, polisi, maofisa ustawi wa jamii pamoja na kada nyingine tangu kuanzishwa kwake.

“Sasa hivi kituo hiki kina jumla ya watoto 41, ambapo wavulana ni 20 na wasichana ni 21na hadi sasa kituo hiki kimenufaisha zaidi ya watoto 600 na wengi wao wapo kwenye fani mbalimbali za ajira,” amesema Faraji.