RC Morogoro, Kilimanjaro watoa ujumbe mzito kumuaga RAS Arusha

Friday February 05 2021
msibanipic

Viongozi mbalimbali wakitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa aliyekua Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Richard Kwitega kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo

By Mussa Juma

Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Loata Sanare na Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Dk Anna Mghwira wamesema pengo aliloacha Richard Kwitega ni kubwa na kuwataka madereva kuwa makini barabarani.

Wakizungumza wakati wakitoa salamu kumuaga aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega ambaye alifariki juzi kwa ajali ya gari wamesema kumpoteza kiongozi huyo ni pengo.

Sanare amesema alifanya kazi na Kwitega alipokuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha alikuwa mtu mwema sana.

"Nilifanya naye kazi alikuwa mtu mwema sana, alikuwa msikivu aliweza kuhimili siasa za Arusha," amesema

Kwa upande wake Dk Mghwira amesema ajali ya Kwitega inatakiwa kutoa funzo kwa madereva kuwa makini barabarani.

Amesema ajali hiyo ingeweza kuepukika kama madereva wangekuwa makini.

Advertisement

"Chanjo cha kifo hiki ni ajali ambayo ingeweza kuepukika, leo tumempoteza kiongozi mwema sana," amesema

Kwitega alifariki akiwa katika safari ya kikazi kwenda Dodoma kuhudhuria vikao vya viongozi wa mikoa.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Mdori Kijiji cha vilima vitatu Wilayani Babati mkoa Arusha baada ya gari lake kugongana na Basi la Makala lililokuwa linatoka Singida kwenda Arusha.

Ibada ya kumuaga Kwitega amefanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha

Advertisement