Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RC Mtwara awapa neno benki kusaidia huduma za afya

Muktasari:

  • Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict ya Ndanda ambayo mwaka 2027 itatimiza miaka 100 imekuwa mkombozi kwa wananchi wengi wa mikoa ya kusini na nchi ya jirani ya Msumbiji.

Mtwara. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas ametoa rai kwa Benki ya NMB kuendelea kufikiria vituo vingine vya afya na hata shule zenye uhitaji, baada ya kutoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict ya Ndanda iliyopo wilayani Masasi vyenye thamani ya zaidi ya Sh15 millioni.

Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vitano vya kulazia wagonjwa wa kawaida pamoja na magodoro yake, mashuka 100, makabati madogo kumi, vitanda vya wagonjwa wasiojiweza vitano, viti vya magurudumu vitano, stendi za kusimamishia dripu kumi na ‘screen’ za hospitali tano.

Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini, Janeth Shango amesema leo Februari 2, 2023 kuwa vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wa Benki ya NMB katika maendeleo ya jamii na Benki hiyo inayo wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida inayopatikana.

“Afya ni moja ya kipaumbele kwa Benki ya NMB na ni kutokana na ukweli kuwa afya ni msingi mkubwa sana kwa maendeleo ya Taifa lolote hapa duniani,” alisema Janeth.

Amesema benki hiyo kama wadau wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo za serikali kwa kusaidia jamii kwani jamii ndiyo imeifanya benki hiyo kuwa hapa ilipo.    

Katibu wa Hospitali hiyo, Joseph Ndukusi Saiburu alisema kuwa msaada wa benki hiyo ni muhimu na umekuja wakati mwafaka ambapo hospitali hiyo inafanyiwa ukarabati mkubwa katika idara karibu zote.

“Tumefanya ukarabati wa wodi nyingi unaoenda kuweka vitanda vya kisasa na hivi vitanda ni gharama, msaada huu umekuja muda mzuri, tuna uhitaji wa vitanda 200 vya kisasa huu msaada umetuongezea nguvu, tuna mpango wa kununua kidogo kidogo kwa sababu ni ghali,” alisema Katibu wa hospitali.

“Hiyo pesa tutapeleka kwenye vitu vingine, tuna upungufu wa screen za hospitali (zile stendi ambazo ziko pembeni ya vitanda) zinaongeza usiri kwa mgonjwa,” alisema.

Amesema Benki ya NMB imewafanyia kitu kikubwa sana kwa vifaa tiba hivyo, na kuongeza kuwa meza za kuhifadhia na kulia chakula walizopewa zitasaidia katika wodi binafsi iliyopo hospitalini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas ametoa rai kwa Benki ya NMB kuendelea kufikiria vituo vingine vya afya na hata shule zilizo katika uhitaji.

Vilevile Kanali Abass ameiomba Benki ya NMB kuendelea kubuni bidhaa na huduma nafuu zaidi ambazo mfanyakazi wa kawaida anaweza kumudu na kuzidi kuboresha huduma kwa wateja hasa watumishi wa afya ili idadi yao iweze kuongezeka jambo ambalo litawapa fursa nyingi zikiwemo kukopa ili wawe na amani wanapokuwa kazini na kuongeza tija kwenye maeneo yao kazini.

“Nawapongeza sana NMB kwa kuchagua kutoa mchango wao wa vifaa tiba hapa Hospitali ya Ndanda iliyopo wilayani Masasi mkoani hapa,” amesema Kanali Ahmed.