RC Tabora apigia debe muhogo unaoongeza nguvu za kiume

RC Tabora apigia debe muhogo unaoongeza nguvu za kiume

Muktasari:

  • Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian amesifia aina mpya ya muhogo ijulikanayo kama Tumbi Tari 4 akisema inaongeza nguvu za kiume.

Tabora.  Mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian amesifia aina mpya ya muhogo ijulikanayo kama Tumbi Tari 4 akisema inaongeza nguvu za kiume.

Akizungumza jana Oktoba 19 wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Lishe inayofanyika Kitaifa mkoani Tabora, Dk Burian amesema aina hiyo mpya imeonekana ina madini mengi ya zinki na hivyo kuongeza nguvu za kiume.

"Mikoa mingine wafahamu kuwa tayari utafiti umefanyika kuhusu aina hiyo ya mihogo," amesema Dk Burian.

Ameongeza kama wanawake watapika mihogo hiyo, wataweza kulinda ndoa zao na kuondokana na migigoro ndani ya nyumba.


Ameeleza kuwa watahamisha ulaji wa vyakula vya asili na kufanya mkoa wa Tabora upunguze udumavu kwa asilimia 10 ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo.

Kwa sasa udumavu kwa mkoa wa Tabora ni asilimia 25 na mkoa umejjwekea mkakati wa kufikia asilimia 15 katika kipindi Cha miaka miwili ijayo.

Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema watatoa elimu kuhusu umuhimu wa lishe na athari zake kwa jamii ili watu waondokane na udumavu a kuwa na Afya Bora.

Kilele Cha wiki ya Lishe kunatarajia kuwa tarehe 23 mwezi huu ambapo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Dorothy Gwajima atakuwa mgeni rasmi.