Ripoti ya CAG yatua bungeni

Thursday April 08 2021
CAG

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere (aliyevaa tai nyekundu) akiwa na maofisa waandamizi wa taasisi hiyo bungeni wakati ripoti zao zilipokuwa zikiwasilishwa bungeni, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

By Habel Chidawali

Dodoma. Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema ataikabidhi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  kwa kamati mbili za Bunge.

Amezitaja kamati hizo kuwa ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac).

Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 muda mfupi baada ya Serikali kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu za wizara, taasisi na mashirika yaliyo chini yao.

Waliowasilisha taarifa ni Wizara ya Tamisemi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya Rais Utumishi.

Mbali na kauli ya Spika, leo CAG ameita waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuzungumzia ripoti hizo.

Advertisement