Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

RPC Kilimanjaro awaonya watakaovunja sheria sherehe za Eid el Fitr

Muktasari:

  • Jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro, limewaonya watakaotumia vilevi wakati wa sherehe za Eid el-Fitr kuwa waangalifu na watakaokiuka sheria za usalama barabarani watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria.

Moshi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limesema litawachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria watakaobainika kuendesha magari huku wakiwa wamelewa na watakaovunja sheria za usalama barabarani wakati wa sikukuu za Eid-el Fitr

Onyo hilo limetolewa leo, Aprili 20, 2023 na Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu Jeshi hilo lilivyojipanga katika sherehe za sikukuu za Eid el-Fitr zinazotarajiwa kufanyika kesho au kesho kutwa.

"Nitoe onyo kwa wote watakaotumia vilevi wakati huu ambao tutakuwa kwenye sherehe za Eid el-Fitr hatutawavumilia endapo watavunja sheria sehemu za starehe, barabarani na maeneo mengine,”amesema.

Aidha, Kamanda Maigwa amesema Jeshi hilo limejipanga kuhakikisha sherehe hiyo inapita salama na watu wanakuwa salama katika maeneo mbalimbali ya misikiti, kumbi za starehe pamoja na barabarani.

"Ndugu zangu tunaelekea katika sikukuu za Eid el-Fitr na katika sikukuu hizi Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro tunaendelea na misako kuwabaini na kuwakamata wahalifu watakaokiuka kanuni na sheria za usalama barabarani.

"Niwatake wananchi wote wa Mkoa wa Kilimanjaro, kuanzia Aprili 21 na kuendelea mwezi unaweza kuandama , kwahiyo Jeshi la Polisi tumejipanga katika maeneo yote ya misikiti, katika barabara zote, watumiaji wa barabara, watembea kwa  miguu tutahakikisha kila mtu anakuwa salama, "ameongeza.

Pia, RPC Maigwa amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha sikukuu hizi zinapita salama. Vijana pamoja na watoto watumie maeneo ya wazi ambayo ni rahisi kuonekana na sehemu yenye hewa ya kutosha katika kusherehekea sikukuu hizi