RPC Manyara aomba wananchi kujenga imani na Jeshi la Polisi

Kamanda wa Jeshi la Polisi Manyara, RPC George Katabazi akiongea na waandishi wa habari leo Jumatatu Mei 22,2023.

What you need to know:

  • Awataka kuondokana na fikra kuwa Polisi hawatendi haki badala yake waendelee kuwa na imani nao na kutoa ushirikiano kwani wanazingatia maadili weledi wa kazi zao.

Babati. Wananchi waondokane na fikra potofu kuwa Jeshi la Polisi halitendi haki, sasa waliamini na waondokane na fikra kwamba Polisi hawawezi kutenda haki na  wababaishaji.

 Kamanda wa Jeshi la Polisi Manyara, RPC George Katabazi akizungumza Leo Jumatatu Mei 22, 2023 mjini Babagi na waandishi wa habari amesema Jeshi hilo limebadilika sasa kwa kiwango kikubwa.

"Tulikamata mali mbalimbali za wizi na wahusika wakiwa na fedha hizo za wizi zaidi ya Sh20 mil mjini Babati Mei 16, 2023 na  nikatoa wito kwa wananchi kujitokeza kutambua mali hizo," amesema.

"Wananchi ongezeni imani na jeshi lenu la Polisi... Mkoa wa Manyara na muondokane na fikra kwamba Polisi hawawezi kutenda haki...kuna baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi sana niwahakikishie kuwa tunatenda haki kazi zetu sasa kunazingatia nidhamu, haki, weledi na uwadilifu mafanikio haya kukamata wahalifu yametokana na kauli mbiu hii," amesema RPC Katabazi.

Tuamini Polisi wetu tujiamini sisi Watanzania tuamini Jeshi la Polisi tuondokane na fikra za zamani kwamba Polisi hawawezi...Polisi ni wababaishaji yawezekana hao uliowahi kukutana nao ni baadhi au mmoja tu lakini Polisi tuliowengi sasa tumebadilika tunafanya kazi kwa kuzingatia weledi na uadilifu mkubwa kama kaulimbiu yetu inavyojieleleza," amesema.

Kamanda Katabazi ametoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kuhusu masuala ya ulinzi shirikishi akisema Polisi ni wachache hivyo kwa kushirikiana na wananchi wanaweza kutanzua na kuzuia uhalifu Mkoa wa Manyara unaoendelea.

Kwa upande wake Juma Musa (mfanyabiashara wa nyama mjini Babati alipongeza Jeshi hilo la Polisi kwa kuokoa mali zake zilizokuwa zimeibwa.

"Mei 16, 2023 tukitoka eneo la machinjioni kuingia ndani ya bucha nilikuta hali tofauti kangalia juu nikaona kumetobolewa…Nikajua kumeibiwa kuangalia panga na shoka tukavikosa nikaenda kutoa taarifa kituo cha Polisi Babati na kupewa RB namba wakati huo majirani zangu nao walibaki kulalamika kuwa wameibiwa," amesema.

Kwa upande wake Imani Hemed alieleza kuwa katika ofisi yake wezi hao walivunja droo na kukagua kila mahali ambapo walikata selfu ya kuhifadhia fedha na kuondoka na zaidi ya Sh20 mil.

Watuhumiwa hao wawili akiwemo mwanamke mmoja walikamatwa wakiwa nyumba ya kulala wageni wakiwa na simu za mkononi 27 pamoja na zaidi ya Sh20 mil.