Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu wabunge Viti Maalum kutoshiriki vikao vya fedha yatajwa

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Kakunda akijibu maswali bungeni katika kikao cha 30 cha mkutano wa Bunge la Bajeti, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda

Dodoma.  Serikali imesema wabunge wa Viti Maalum hawaingii katika  vikao vya kamati za fedha za halmashauri wanazotoka kwa sababu ya kutotajwa kwenye  sheria iliyoainishwa na kifungu cha 41(1) na kifungu cha 40 (2)cha kanuni za kudumu za Serikali za Mitaa.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kakunda ameliambia Bunge leo Mei 16, 2018 kuwa kanuni za Serikali za Mitaa za mwaka 2014, zinafafanua mahitaji ya sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka ya wilaya) sura 287, kifungu cha 75 na sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za miji) sura ya 288 kifungu cha 47.

Kakunda ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum (CCM), Taska Mbogo aliyehoji kwa nini wabunge wa viti  maalum hawaingii kwenye vikao vya kamati za fedha za halmashauri zao.

Katika ufafanuzi wake, Kakunda amesema kamati ya fedha, uongozi na mipango imeundwa kwa mujibu wa sheria na inawataja wajumbe kuwa ni meya au mwenyekiti wa halmashauri ambaye atakuwa ni mwenyekiti.

Wengine ni naibu meya au makamu mwenyekiti, mbunge au wabunge wa majimbo, wenyeviti wa kamati za kudumu na wajumbe wengine wasiozidi wawili.

Amesema kwa sasa utaratibu utaendelea hivyo ikiwemo kutokutoa fedha za mfuko wa jimbo kwa wabunge wa viti maalum hadi hapo sheria itakapobadilishwa.