Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sabaya afikishwa Mahakama Hakimu Mkazi Moshi leo

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akishuka kwenye karandinga wakati alipofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi leo,  Aprili 5,2023. Picha na Janeth Joseph

Moshi. Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amefikishwa kwa mara nyingine tena leo April 5, 2023  katika Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi.

Juni Mosi, 2022 Sabaya na wenzake wanne  walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wakikabiliwa na mashtaka 7 ikiwemo uhujumu uchumi.

Septemba 6 mahakama hiyo iliwaachia huru washtakiwa wanne, Sylivester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey baada ya kukiri kutenda makosa ambapo mahakama  iliwatia hatiani na kuwaamuru kulipa kila mmoja faini ya Sh50,000 na fidia ya Sh1 milioni kwa waathirika wa tukio hilo ambaye ni Alex Swai.

Hata hivyo, Machi 29, mwaka huu alipofikishwa mahakamani hapo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Sabitina Mcharo aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo namba mbili ya mwaka 2022 umekamilika na kuiomba mahakama hiyo kuwapa tarehe ya karibu kwa ajili ya kuweka vibali pamoja na kuendelea na taratibu nyingine kwa mujibu wa sheria.