Wenzake Sabaya watiwa hatiani, wakubali kulipa Sh1 milioni

Sabaya na wenzake wakitoka ndani ya mahakama baada ya kesi yao kuahirishwa mpaka Agosti 12, 2022. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Washtakiwa hao wamekukubali kulipa faini Sh50, 000 kila mmoja na kumlipa Mhanga Alex Swai Sh1 milioni kila mmoja.

Moshi. Washtakiwa wanne kati ya watano katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya wametiwa hatiani baada ya kukiri kutenda makosa mawili.

Washtakiwa hao wamekukubali kulipa faini Sh50, 000 kila mmoja na kumlipa Mhanga Alex Swai Sh1 milioni kila mmoja.

Washitakiwa hao ni Sylvester Nyegu, John Aweyo, Nathan Msuya na Antero Assey ambapo wamekutwa na makosa mawili leo Jumanne, Septemba 6, 2022 katika Mahakama ya Hakimu MakaziĀ  Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Mashtaka yao moja kujitwalia madaraka isiyovyo halali na kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwa Alex Swai na kosa la pili kula njama na kumnyima na kukandamiza haki ya mhanga ambaye ni Alex Swai kwa madai ya kukwepa kulipa kodi.

Hata hivyo, washatakiwa hao kwa pamoja mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Salome Mshasha wamekubali kulipa Sh1,050,000 kwa kila mmoja.

Kwa undani wa habari hii endelea kufuatilia Mwananchi.