Safari za treni ya abiria, mizigo zarejea

Muktasari:

  • Safari za treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) zimerejea kama awali baada ya kusimama kwa muda kutokana na ubovu kati ya stesheni ya Gulwe na Godegode mkoani Dodoma.

Dodoma. Safari za treni ya Shirika la Reli Tanznaia (TRC) zimerejea kama awali baada ya kusimama kwa muda kutokana na ubovu kati ya stesheni ya Gulwe na Godegode mkoani Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Januari 21, 2021 msemaji wa TRC,  Jamila Mbarouk amesema safari zimerejea baada ya kusimama kwa muda na kusababisha abiria kutumia mabasi  kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro kuelekea Dodoma, Tabora, Shinyanga na Mwanza.

"Njia ilishafunguka hakuna tatizo kwa wakati huu na usafiri umerejea kawaida...,tuwaombe wateja wetu waendelee kutuunga mkono nasi tukiendelea na maboresho kila wakati," amesema Jamila.

Tangu kuanza kwa safari hizo idadi ya abiria katika stesheni ya Dodoma imepungua.