Sakata la Kajala, Mobetto upelelezi unaendelea

Sakata la Kajala, Mobetto upelelezi unaendelea

Muktasari:

  • Jeshi la polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa sakata la kusambaa kwa video za Paula na msanii Rayvanny.

Dar es Salaam. Jeshi la polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa sakata la kusambaa kwa video za Paula na msanii Rayvanny.

Hayo yameelezwa jana Ijumaa Februari 26, 2021 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kangai alipoulizwa na Mwananchi Digital kuhusu lilipofikia sakata hilo.

Februari 16, 2021 Kajala alipewa saa 12 kukanusha tuhuma alizomtupia mwanamitindo, Hamisa Mobetto kwamba alimkutanisha Paula na Rayvanny siku aliyodai mwanaye huyo alinyeshwa pombe na kurekodiwa video za ngono.

Mwanasheria wa mwanamitindo huyo, Elia Rioba alieleza kuhusu Kajala kutakiwa kukanusha ikiwa ni takribani siku mbili tangu amtuhumu Mobetto. Hata hivyo Kajala hakukanusha maelezo yake hayo.

Kajala ambaye kwa sasa yupo katika mahusiano na msanii Harmonize alitoa tuhuma hizo Jumapili Februari 14, 2021  kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram yenye wafuasi milioni 4.4, na baada ya muda Mobetto alimjibu kupitia ukurasa wake wa Instagram pia.

Baadaye Kajala alipeleka sakata hilo polisi na Mobetto kutakiwa kuripoti kituo cha polisi Kawe na baadaye suala hilo kuhamishiwa kituo cha polisi Oysterbay.

Katika maelezo yake Kangai amesema bado wanafanya upelelezi na utakapokamilika wahusika watafikishwa mahakamani.