Sakata la shehena ya mahindi, RC Shigella asema hali ni shwari

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amesema shehena za mahindi kutoka Tanzania kwenda Kenya zinapitishwa katika mpaka wa Horohororo bila vikwazo ambapo kuanzia Machi 5 hadi 7 mwaka huu jumla ya tani 510 zimepitishwa mpakani hapo.

Tanga/Dar. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amesema shehena za mahindi kutoka Tanzania kwenda Kenya zinapitishwa katika mpaka wa Horohororo bila vikwazo ambapo kuanzia Machi 5 hadi 7 mwaka huu jumla ya tani 510 zimepitishwa mpakani hapo.

Hata hivyo, zuio la kupeleka mahindi Kenya lilitolewa juzi na Wakala ya Kilimo na Chakula ya nchi hiyo ikidai kuwa mahindi kutoka Tanzania na Uganda yana kiwango kikubwa cha sumu kuvu ambayo ni hatari kwa usalama wa walaji.

Jipatie nakala yako ya gazeti la Mwananchi leo Machi 08, 2021 ili kujua undani wa habari hii