Samia: Endesheni bodaboda mkiwa na mikataba, si kuwanufaisha matajiri

Muktasari:

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha bodaboda kutofanya kazi hiyo kwa kuwanufaisha matajiri na badala yake wafanye kwa mikataba.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amewataka waendesha bodaboda kutofanya kazi hiyo kwa kuwanufaisha matajiri na badala yake wafanye kwa mikataba.

 Akizungumza barabarani na wakazi wa Mwanza baada ya kuwasili mkoani humo kwa ziara ya siku tatu leo Jumapili Juni 13, 2021 amesema, “bodaboda nadhani mmesikia nilivyowafanyia kwenye bajeji sasa naomba  muache kuwanufaisha matajiri.”

“Endesheni kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya hapo pikipiki ibaki kuwa yako uendelee na kazi ili  hizi fursa zinazotolewa na Serikali kwa bodaboda ziwafikie wahusika.”

Pia Rais Samia amewataka wamachinga kufuata sheria, miongozo na taratibu zinazowekwa na halmashauri ili waweze kufanya biashara zao bila kubughudhiwa.