Serikali kusaka kodi za wamiliki wa mitandao

Serikali kusaka kodi za wamiliki wa mitandao

Muktasari:

  • Serikali ya Tanzania imesema inafanya maandalizi ya kuwatoza kodi wamiliki wa mitandao ya kijamii ikiwemo Google,Twitter,Facebook,Instagram, apple kama nchi zingine zinavyofanya.

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema inafanya maandalizi ya kuwatoza kodi wamiliki wa mitandao ya kijamii ikiwemo Google,Twitter,Facebook,Instagram, apple kama nchi zingine zinavyofanya.

Kauli hiyo imetolewa leo, Jumatano, Septemba Mosi, 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati alipokuwa akizungumzaia marekebisho ya tozo katika miamala ya simu yaliyofanywa na Serikali.

 “Biashara zinahamia kidijitali, kuna ‘components’ kubwa inayofanya biashara kwa njia za kimtandao. Zile biashara zilizohamia kwenye mtandao hakuna eneo zinazotozwa kodi,” 

Dk Mwigulu amesema, “tozo sio adhabu bali ni mshikamano kwa sababu kuna watu wetu wana uhitaji, nilivyoingia niliwaambia watalaamu mbona haya makubwa makubwa tunayaacha? Kwa hiyo tunaangalia namna hivi App vikubwa vikubwa ambavyo tukishika simu zenu mnavitumia, jamaa anakusanya fedha huko huko hapa hana ofisi.

“Au mnaviona vipo katika simu tu, kuna majamaa yanatengeneza fedha, si mmeshavielewa kila kimoja? Ukiondoa vile vyenye namba ya simu vile vingine ambavyo ukibonyeza unaweza kucheza au muziki subscribe. Vipo vingi lakini kodi yake imelipiwa wapi,”amesema Dk Mwigulu.

Dk Mwigulu amesema ameshazungumza na wataalamu wake, kuhusu suala hilo na kwamba  wanalilia ‘timing’ hata kama wahusika hawana ofisi hapa nchini,  lakini kwa kuwa  teknolojia inakua hawatashindwa kuwapata hata mahali.

“Biashara zinahamia mtandaoni, tunataka tuone namna ya kupata hii huduma ya kodi kwa njia ya mtandao. Nimewaambia waendelea kuangalia nchi zilizofanikiwa ili tuone namna ya kuichukua.