Serikali kutoa mbegu za alizeti kwa ruzuku

Sunday June 13 2021
mbegu pic
By Noor Shija

Singida. Serikali imesema ina mpango wa kuanza kutoa ruzuku ya mbegu bora kwa mfumo wa ruzuku.

 Hayo yamesemwa leo Juni 13, 2021 na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akitoa mkakati wa Serikali wa kuhakikisha mbegu za alizeti zinapatikana kwenye mkutano wa kampeni ya kitaifa ya kilimo cha alizeti.

"Mbegu bora za alizeti zitatolewa kwa mfumo wa ruzuku ya asilimia 50 na Serikali. Aidha, malipo ya mbegu hizo yatafanyika mwishoni mwa msimu wakati mkulima anauza alizeti," amesema Bashe.

Bashe amesema wizara itaandaa mwongozo wa utekelezaji utakaoainisha majukumu ya kula mdau.

Ametaja mwongozo huo kuwa mkulima atakuwa na jukumu la kuzalisha alizeti, jukumu la kutoa mbegu na ruzuku litafanywa na wizara.

Amesema wasindikaji watakuwa na jukumu la kununia alizeti kutoka kwa wakulima.

Advertisement

"Tamisemi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi jukumu lao ni kusimamia mfumo wa kilimo cha mkataba," amesema Bashe.

Pia, amesema kampuni binafsi za mbegu zitakuwa na jukumu la kushirikiana na ASA (Wakala wa Mbegu za Kilimo Tanzania) kuhakikisha kunakuwep upatikanji wa Mbegu bora.

"Taasisi za kifedha nazo zitakuwa na jukumu la kugharamia upatikanji wa mbegu bora kwa kushirikiana na Serikali," amesema Bashe.

Amesema kila hatua ya utekelezaji itakuwa na mkataba kwa upande zote za utekelezaji


Advertisement