Serikali ya Tanzania yakamilisha malipo ya ndege tatu

Tuesday April 13 2021
ndege pc
By Mwandishi Wetu

Dodoma.  Serikali ya Tanzania imesema imekamilisha  malipo  ya ununuzi  wa  ndege mpya tatu, mbili zikiwa ni Airbus A220-300 na moja ni Dash    8-Q400De-Havilland.

Hayo yamesema leo Jumanne Aprili 13, 2021 bungeni mjini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha bungeni mwelekezo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2021/22.

Amesema ndege hizo zinatarajiwa  kuwasili kati ya mwaka 2021 au 2022 na hivyo kuwezesha  Serikali  kuwa  na jumla  ya  ndege  12.

“Nitumie fursa hii kulipongeza Shirika la Ndege Tanzania    kwa    kuanzisha safari za  kwenda Guangzhou, China,” amesema Majaliwa akibainisha kuwa safari hizo zitakuwa chachu ya kuimarisha biashara, utalii na ajira.

Advertisement