Advertisement

Serikali yaagiza Askofu Gwajima kukamatwa

Tuesday August 17 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

IN SUMMARY

  • Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dk Dorothy Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini  ( Takukuru)  kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli  anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi  kuhusu chanjo   ya Uviko 19.
Advertisement

Butiama. Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Dk Dorothy Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini  ( Takukuru)  kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli  anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi  kuhusu chanjo   ya Uviko 19.

Soma zaidi:  Askofu Gwajima aitahadharisha Serikali kuhusu chanjo za corona

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne  Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa  Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi  jambo linaloivuruga   wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Soma zaidi: Dk Gwajima: Sijutii kujifukiza kujikinga na corona


Kwa muda sasa Askofu Gwajima amekuwa akisisitiza kuwa hatakubali kupatiwa chanjo ya kukabiliana na Uviko-19 na kuwataka waumini wake kutojitokeza kwenda kuchanja.

Askofu Gwajima ametoa msimamo huo wakati Spika wa Bunge, Job Ndugai akiwaasa wabunge kujitokeza kuchanja na kwamba japo ni hiyari lakini hakuna hiyari ya kuwaambukiza wengine Uviko-19.

Advertisement
More From Mwananchi
This page might use cookies if your analytics vendor requires them.