Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh142 milioni zakopeshwa vijana, wenye ulemavu Hai

Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe akikata utepe wakati akikabidhi bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu (guta) kwa vijana, akina mama na watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Vikundi 14 vya vijana, kina mama na wenye ulemavu katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro wamepatiwa mkopo wa zaidi ya Sh142 milioni ili kujikwamua kiuchumi.

Hai. Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe amewataka wanufaika wa mikopo inayotolewa na halmashauri hiyo, kuwa waaminifu na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati huku akimwomba mkuu wa wilaya hiyo kuwachukulia hatua wale watakaokaidi kurejesha mikopo hiyo.

Amesema katika wilaya hiyo, ipo changamoto ya urejeshwaji wa mikopo inayotolewa kwa makundi hayo hali ambayo inafanya baadhi ya wanufaika wengine kushindwa kupata  mikopo hiyo kwa wakati.

 Akikabidhi mikopo hiyo zikiwemo fedha taslimu, bodaboda na pikipiki za magurudumu matatu (guta) yenye thamani ya zaidi ya Sh142 milioni   kwa vikundi 14, Mbunge Mafuwe amewataka kuwa wazalendo na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.

"Leo tunakopesha Sh142 milioni ambayo ni asilimia 10 ya mapato yanayokusanywa ndani ya Halmashauri ya Hai. Hiombe, hii mikopo mliyopewa leo inapaswa kurejeshwa kwa wakati, hii ni mikopo sio zawadi,” amesema Mafuwe.

 "Mimi nitamwomba mkuu wa wilaya atusaidie kudai wale ambao watakuwa wazito kulipa. Hapa tumeambiwa changamoto ni kwamba watu hawaleti marejesho. Hii sio sawa niwaombe ninyi ambao mnakabidhiwa mikopo hii leo muwe waaminifu, mlete marejesho ili na wengine wapate,” amesema

 “Hatutegemei kusumbuana na ninyi kwenye marejesho, tunategemea mrejeshe kwa wakati lakini ni vizuri mkakaa karibu na maofisa maendeleo ya jamii ili mpate ushauri ili uwaongoze namna ya kutunza na kuendesha biashara zenu,” amesema.

 “Tunategemea ninyi mzalishe ajira zaidi, leo tunakabidhi vikundi 14 na wenyewe wakaongeze vikundi vingine ndani ya vikundi watu waweze kupata ajira lakini pia na uchumi wa mtu mmoja mmoja uweze kukua,” amesema.

 Ofisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Robert Mwanga amesema mwaka 2021/22 halmashauri hiyo ilitoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Sh432.5 milioni huku akisema changamoto kubwa iliyopo ni ucheleweshaji wa marejesho.

"Katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2022 tumefanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya Sh142.3 kati ya fedha hizo Sh42 milioni zilitokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani na Sh99.6 milioni zilitokana na fedha za marejesho," amefafanua.

Amesema kumekuwepo na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanufaika wa mikopo kutokurejesha kwa wakati kutokana na dhana kwamba ni fedha za serikali na hivyo hazipaswi kurejeshwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo, Wanguba Maganda ameitaka Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhakikisha pindi wanapotoa mikopo wahakikishe wanaowapa mkopo ni watu sahihi.

"Idara ya Maendeleo ya Jamii, ninawasihi na ninawaomba kwamba wakati wote kabla ya kutoa mikopo, mhakikishe hawa watu mnaowapa mkopo ni watu hai, tangu mnampa mkopo mpaka anaporejesha mikopo,"amesema.

Richard Ndosi mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, ameishukuru serikali kwa kuwafikia  na kwamba watarejesha mikopo hiyo kwa wakati ili iweze kunufaisha wengine.

"Tunaishukuru serikali kwa kutupatia mikopo sisi vijana, hatutawaangusha kwenye suala la urejeshaji wa mikopo hii," amesema Ndosi.