Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh67.4 bilioni kuendeleza vijana Kigoma

Muktasari:

  • Wasichana na wavulana walio katika mazingira magumu katika Wilaya za Mkoa wa Kigoma kunufaika na mradi wa Wezesha Binti unalenga kuwasaidia kupata elimu ya sekondari na mafunzo katika mazingira salama itakayochochea kufikia ndoto zao.

Dar es Salaam. Mradi wa Wezesha Binti unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (Enabel) unakusudia kutumia euro 25, 000, 000 (takribani Sh67.4 bilioni), kuwasaidia Wasichana na Wavulana kuanzia miaka 14 hadi 29 walio katika mazingira magumu katika wilaya za Mkoa wa Kigoma.

Msaada huo ambao utadumu kwa miaka mitano, utawawezesha kupata mahitaji muhimu ili wafanikiwe kumaliza elimu ya sekondari kwa ufanisi na kupata ujuzi wa kufikia ndoto zao.

Akizungumza Dar es Salaam, leo Jumatano Desemba 6, 2023 wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mwakilishi Mkazi wa taasisi hiyo nchini, Koenraad Goekint amesema pia mradi huo utaboresha miundombinu kwa baadhi ya shule za Sekondari na kuwajengea  uwezo walimu katika masomo mbalimbali ikiwemo hisabati, sayansi na tehama.

"Tunataka vijana wamalize elimu ya sekondari na ujuzi utakaowasaidia kupata ajira bora na endelevu na kama wanaingia kwenye ujasiriamali wawe wamenolewa katika maarifa sahihi katika mazingira yenye usawa wa kijinsia," amesema Goekint.

Amesema mradi utashirikiana na vyuo husika katika kutoa mafunzo ya ufundi stadi yanaoendana na mahitaji ya soko la ajira kwa lengo la kutengeneza kundi la vijana wajasiriamali na wenye uwezo wa kutengeza ajira zao na za wengine.

"Miradi utashirikiana na wadau mbalimbali katika kukabiliana na changamoto zinazosababisha kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia kwa nia ya kuwasaidia wasichana kufikia malengo yao ya kielimu na kiuchumi," amesema Goekint.

Mhadhiri wa Mafunzo ya Maendeleo, Dk Lilian Victor Mtasingwa amesema mpango huo utachochea hamasa kielimu kwakuwa walio wengi wanashindwa kutokana na changamoto mbalimbali.

"Wanapitia changamoto nyingi za mila na desturi lakini kutoka na mpango huu naamini jamii hasa za vijijini zitapata hamasa kubwa," amesema.

Awali, Ofisa Mshauri wa Mikakati ya Wanawake wa Umoja wa Mtaifa nchini, Usu Mallya amesema mpango huo utachochea hata kubadilika kwa kanuni za viongozi wa mitaa, wanajamii na familia na wanawake vijana na kujua kuhusu haki na huduma.

"Taasisi ina taarifa, maarifa na ujuzi unaohitajika ili kutetea uwezeshaji wa wanawake Kigoma na kutoa huduma zinazozingatia jinsia," amesema.