Shahidi aeleza mawasiliano ya Mbowe katika kesi ya ugaidi

Tuesday January 18 2022
mboweeepic
By Fortune Francis
By James Magai

Dar es Salaam. Mtaalamu wa uchunguzi wa uhalifu wa kimtandao wa jeshi la polisi, Innocent Ndowo ameeleza mawasiliano kati ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Luten Denis Urio yalivyokuwa.

Shahidi huyo wa 10 wa upande wa mashtaka katika kesi ya ugaidi inayomkabili  Mbowe na wenzake watatu amedai amebaini ujumbe mfupi uliotoka kwa Urio kwenda kwa Mbowe akitaka atume Sh500,000 kwa ajili ya kuwasafirisha mshtakiwa wa kwanza na wa pili.

Soma ushahidi hapa

Sasa Jaji Tiganga ameingia mahakamani na kesi inatajwa na karani.

Waendesha mashtaka wanajitambulisha wakiongozwa na kiongozi wao Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando

Jopo la mawakili wa utetezi likiongozwa na Peter Kibatala linajitambulisha.

Advertisement

Jaji anawaita washtakiwa kwa namba zao kuanzia wa kwanza hadi wa nne kujiridhisha Kama wote wako mahakamani nao wanaitika mmoja mmoja.

Wakili wa Serikali Kidando: Mheshiwa Jaji kesi imekuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa na shahidi tuliyekuwa naye jana amefika na ametutaarifu kuwa hali yake imeimarika na anaweza kuendelea. Tuko tayari kuendelea

Jaji:Utetezi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia tuko tayari kuendelea

Jaji:Shahidi nakukumbusha uko chini ya kiapo tangu jana.

Wakili wa Serikali  Mwandamizi Pius  Hilla anaendelea kumwongoza shahidi kutoa ushahidi wake kuanzia alipoishia Jana.

Jaji: Anarejea mahali ilipoishia jana kisha wakili anaendelea kumwongoza shahidi naye anaeleza

Shahidi: Ripoti yangu kwenda kwa wapelelezi iliambatana na covering letter kutoka Police Forensic Bureau. Covering letter inaandaliwa na mchunguzi Kisha inakwenda kwa kamishna Msaidizi wake anasaini kwa niaba.

Madhumuni ya covering letter ni kutambulisha kazi iliyofanywa na mchunguzi.

Shahidi: Extracted information zilitokana na vile vilelezo vilivyoletwa maabara yaani simu nane lakini simu nne ndizo zilikuwa na matokeo positive ambazo ya kwanza niliipa alama ya herufi E, kwenye stika ya kijani ambayo ni aina ya Tecno.

Shahidi: Nyingine niliipa alama F kwa mkono wangu ambayo ni aina ya Itel.

Shahidi: Simu ya tatu niliipa alama G, aina ya Tecno

Shahidi: Simu ya nne niliipa alama H, Tecno.

Shahidi: Alama hizi nilikuwa naziweka nyuma ya simu na zile ambazo zilikuwa na cover nilikuwa naweka kwenywe cover na nyuma ya simu.

Shahidi: Nilikuwa naweka alama kwenye simu kwa ajili ya utambuzi wangu wakati nafanya Uchunguzi.

Shahidi: Barua hiyo ya co erring letter nitazitambua kwa nembo ya ofisi, saini ya SACP Naftali Joseph Mwamtamba, mhuri wa Kamishina,

Shahidi: Ripoti yangu nikioona nitaitambua kwa logo ya taasisi yetu, Jeshi la Polisi, majina yangu, saini yangu, mhuri wa Jeshi la Polisi

Shahidi: Simu niiyoipa alama E niliona nitaitambu kutokana na IME za kiuchunguzi lakini ni naomba mahakama inielewe namba za IMEI ni 14 hadi 15 15 kwahiyo nichofanya ni kushika baadhi ya namba za mwanzo na mwisho 35 na namba za mwisho 45

Shahidi: Kigezo cha pili cha kutambua ni taarifa zilizoko kwenye report kwanza itakuwa na mhuri wa Polisi, sahihi yangu laboratory namba.

Shahidi: Kigezo kingine kitakuwa kuna majina yangu pia kwa maana ya mchunguzi.

Shahidi: Kigezo kingine ambapo ripoti zinatokana na cerebrate (mashine ya Uchunguzi) pia Kuna kuwa na neno cerebrate

Shahidi: Extracted report ya simu H nitaitambua kwa IMEI yake namba za mwanzo ni 35, saini yangu, mhuri wa Police Forensic Bureau Dar es Salaam, Lab number FB/Cyber/ 2020/476,  majina yangu na neno Cerebrate.

Shahidi: Taarifa kwenye ripoti hizo ni kama vile zilivyokwenye vifaa husika kwa sababu wakati wa extracted na analysis mifumo hii ina teknolojia ambayo hairuhusu kufanya manipulation yoyote, hivyo tekonolojia hiyo inasaidia standard na hivyo ushahidi huo unakuwa uko intact.

Wakili Hilla: Mheshimiwa Jaji kwa kuwa shahidi amesema anao uwezo wa kutambua nyaraka hizo kumuonesha ili aweze kuzitambua

Wakili Hilla: Shahidi naomba utazame nyaraka hizi.

Shahidi anapekuapekua baadhi ya nyaraka alizopewa.

Wakili Hilla: Ieleze mahakama nyaraka hizo ni kitu gani?

Shahidi: Nyaraka hizi Mheshimiwa ni nyaraka ambazo nimeziandaa mwenyewe na nazitambua kuwa ni ripoti ya uchunguzi nilioufanya.

Wakili: Katika ripoti hiyo Kuna nyaraka zipi?

Shahidi: Kuna covering letter, Kuna taarifa niliyoiandaa.

Wakili: Jana shahidi ulieleze annexures kwenye ripoti yako ni zipi hizo?

Shahidi: Taarifa kutoka Airtel na Tigo.

Wakili: Jana uliongelea annexures hizo ziko wapi?

Shahidi: Zilitolewa hapa mahakama

Wakili: Hebu ieleze Mahakama covering letter umeitambua vipi?

Shahidi: Kuna mhuri wa Kamisha wa Uchunguzi, jina la jalada

Wakili: Taarifa yako ina vigezo gani?

Shahidi: Kuna Lab number F? Cyber/2020/.. 479 pamoja na case no., Majina yangu, saini yangu na mhuri wa Police Forensic Bureau

Wakili Hilla: Itazame extracted report ya simu ya alama E, na ieleze mahakama umeitambua?

Shahidi: Ni hii hapa na IMEI kama nilivyozitaja, mhuri wa Police Bureau Dar, saini yangu majina yangu na Lab no.,  fB/Chber/202/Lab/479 pamoja na neno cerebrate

Wakili Hilla: Sasa twende extracted report ya simu namba H unaitambuaje?

Shahidi: IMEI ni, mhuri wa Police Bureau Dar, majina yangu, saini, Lab number na neno cerebrate.

Wakili Hilla: Sasa twende extracted report ya simu namba E unaitabuaje?

Shahidi: kwa IMEI number yake, mhuri wa Tanzania Police Forensic Bureau, majina yangu na Lab number

Wakili Kibatala anasimama na kusema Mheshimiwa nimeshamnong'oneza Wakili Hilla lakini naona bado mambo ni yale yale tu, shahidi anasoma content

Wakili Kidando: Shahidi yuko katka utambuzi na taarifa hizi alishazitaja.

Kibatala: Ndio anasoma na Lab number?

Kidando: Mheshimiwa hizo tayari shahidi alishazitaja.

Jaji nakumbuka wakati akieleze kuwa anazitambuaje nyaraka hizo alisema kwa IMWI numbe na Lab number.

Wakili Hilla: Kwa maana ya utambulisho wa ripoti alizoziandaa anataja alama au vigezo vilivyopo Kama alivyovitaja, kwa hivyo kwa kutaja IMEI number ya kwanza na ya mwisho sidhani kama ana- violate admissibility ya exhibits

Jaji: Napata changamoto kwa sababu anachokisema shahidi ni reference ya kile alichokuwa amekitaja.

Kibatala: Kwa ruhusa yako acha tuendelee maana si kitu kikubwa saana.

Jaji: Na naona alikuwa anaelekea kwenywe kielelezo cha mwisho.

Kibatala: Sawa Mheshimiwa, acha tuendelee.

Jaji anakumbusha shahidi alikokuwa amefikia kisha Wakili Hilla anaendelea kumuongoza shahidi.

Wakili Hilla: Shahidi, Sasa unaiomba nini mahakama, kuhusu nyaraka hizo?

Jaji Tiganga: Hebu ngoja kwanza, ziko ngapi hizo nyaraka? Maana kuna nyaraka ya mwisho ya extracted report H ndio alikuwa anaimalizia.

Kwa mwongozo huo wakili Hilla anamuongoza shahidi kutaja vigezo vya kuitambua ripoti hiyo naye shahidi anavitaja kama alivyokuwa ameshavitaja awali

Wakili Hilla: Shahidi sasa baada ya utambuzi huu sasa unaiomba mahakama ifanye nini

Shahidi: Mheshimiwa naomba nyaraka hizi zipokewe kama ushahidi wangu.

Wakili: Hilla, Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba nyaraka hizi ambazo ameshazitambua zipokewe.

Mawakili wa utetezi wanazipitia nyaraka hizo, ili watoe maoni au msimamo wao kabla ya mahakama kuzipokea.

Wakili Nashoni Nkungu: Mheshimiwa Jaji kwa niaba ya mshtakiwa wa kwanza (Halfan Bwire Hassan) sina pingamizi

John Mallya kwa niaba ya mshtakiwa wa pili (Adamu Hassan Kasekwa) hatuna pingamizi

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa kwa niaba ya mshtakiwa wa tatu( Mohamed Ling'wenya) hatuna pingamizi

Peter Kibatala: Kwa niaba ya mshtakiwa wa nne (Freeman Mbowe) Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi

Jaji Tiganga: kielelezo chenye covering letter ya Police Forensic Bureau

Repoti ya uchunguzi, Extracted report ya simu nne vyote vipokelewa kuwa 22 mpaka 27.

Baada ya vielelezo hivyo kupokewa sasa shahidi anaanza kusoma yaliyomo ndani ya ripoti hizo.

Taarifa ya Uchunguzi:

Shahidi: 13/8/2020 Maabara ya uchunguzi wa Kisayansi ikipokea barua na vielelezo simu nane pamoja na simu card zake kwa ajili ya uchunguzi kubaini Mawasiliano kupitia mitandao ya kijamii Kama vule Whatsapp, Telegram, unumbe mfupi na kupiga nakupigiwa katika namba za simu zilizotangulia, usajili wa namba hizo na Mawasiliano mengine

Kisha shahidi anasoma matokeo ya uchunguzi wake.

Shahidi: Katika uchunguzi huo shahidi anabainisha jinsi namba za simu hizo ambazo amebainisha usajili wake kuwa ni za baadhi ya washtakiwa, hususan Mbowe pamoja na shahidi mtarajiwa wa Jamhuri, Luten Denis Urio, wakijadiliana kuhusu kuwapata vijana ambao wengine  wametajwa miongoni mwa washtakiwa.

Shahidi: Ripoti ya uchunguzi huo inabainisha muda wa mawasiliano hayo kupitia mitandao ya kijamii, zote ujumbe mfupi wa maneno, kupiga na kupokea simu na miamala ya fedha huku mmoja akimtahadharisha mwingine kuwa asiwe anatumia namba yake binafsi kwa masuala ya pesa

Wakati Shahidi anaendelea kusoma taarifa hizo, Jaji anahoji kama kuna kusoma taarifa zote hizo na hasa viambatanisho. Anashauri isomwe ripoti ya uchunguzi na wakili Hilla anamuongoza kwenye maneo muhimu ya uchunguzi.

Shahidi anabainisha mawasiliano Kati ya Mbowe na Denis Urio kuanzia Januari 2020 jinsi walivyotafutana kwa njia ya ujumbe wa mitandao na ujumbe na call kupitia telegram na ujumbe wa maneno

Shahidi: 20/7/2020 saa 1:59 asubuhi kupitia telegram Mbowe anasema kaka wale mtu tatu au nne ni muhimu sana siku zimekwisha.

Shahidi: Baadaye alipiga simu kwa telegram

Shahidi: Saa 1:45 asubuhi Denis alimpigia Mbowe

Shahidi: Saa 1:47'46 Mbowe alimpigia Denis

Shahidi: 20/7/2020 saa 2;20 Denis amtumia Mbowe ujumbe, bro kuna memba wawili mmoja yuko Tunduma anashughulika na mabasi ya safari za nje na mwingine yuko Dodoma

Shahidi:Mboye baadaye simu siyo salama

Shahidi: Baadaye Mbowe atuma ujumbe hao wawili kuanzia siyombaya na hawawezi kutelekezwa wameshakwanbia mahitaki yao

Shahidi: Denis anamtumia Mbowe ujumbe mmoja kazaliwa 1980

Shahidi: Baadaye Denis ujumbe kwa Mbowe nitumie nauli ya kwenda nao Moro

Shahidi: Mbowe anajibu hakuna tatizo, kiasi gani

Shahidi: Denis anajibu laki 5

Shahidi: Saa 2:21:48, Mbowe anajibu sawa kaka

Shahidi: 2:22:29 Denis kwa Mbowe Nashukuru nitakujibu jioni

Shahidi: Denis usiwe unatumia namba yako binafsi kutuma pesa tumia wakala au mtu mwingine

Shahidi: Mbowe Ok

Shahidi: 27/7/2020. Denis yule jamaa anayefanya kazi Yard ameshafika

Shahidi: Yule mtu wa Tunduma anakaribia Moro

Shahidi: Denis Ila Kuna maswali wanauliza kuhusu malazi na mishahara yao.

Shahidi: Baadaye Denis ampigia Mbowe

Shahidi: 22/7/2020 : 6:26  Denis ampigia Mbowe

Shahidi: 2/7/2020 saa 6: Denis Shikamoo mkuu wale vijana tayari niko nao nimekutana nao na wako tayari kwa kazi

Shahidi: Denis naomba unipe utaratibu wao

Shahidi: Mbowe 7:38 Denis amtumia Mbowe kuwa wamekuja Dar anaomba nauli na mahali pa kukutana

Shahidi: 22/7/2020 saa7:51 Denis kwa nauli na chakula kwa wote ni Sh200.000

Shahidi: Mbowe natuma namba gani

Shahidi: Denis 0787555200

Shahidi: Mbowe ni namba ya nani?

Denis: Namba yangu

Shahidi: Denis uliyotumia juzi

Shahidi: Denis Lakini wewe usitumie namba yako

Shahidi: Mbowe: Ok

Shahidi: Mbowe wakiwa around Mlandizi watume sms wanafika muda gani nitatuma gari kuwapokea Ubungo

Shahidi: Denis: niwape namba gani muweze kuwasiliana?

Shahidi: Siku hiyo 3 Mbowe namba ninayotumia unumbe ni ya dereva wangu wamtafute yeye

Shahidi: Denis sawa, nitumie hiyo namba baadaye Denis

Shahidi: Tayari nimeipata

Shahidi: Denis: Nashukuru nimeelewa nitawapa hiyo namba.

Shahidi: Saa 12:20 jioni Denis: Tayari wameshaondoka wanakaribia Ruvu

Shahidi: Denis wale vijana wengine nimewapata Mwanza, Mtwara na Dodoma

Shahidi: Denis: Naomba kushauri uwe unanitumia fedha za kutosha kwa ajili ya ku-mobilize

Shahidi: Mbowe: kaka bado niko kamati kuu tuma ujumbe please.

Shahidi: Denis: Kuna MSG nilizokutumia kuhusu wale vijana wengine ambao wako tayari.

Shahidi: 13/7/2020 Denis: Naomba rejea msg zangu za jana usiku

Shahidi: 23/7/2020 saa 1:03 jioni Urio anapokea ujumbe  wenye jina la Mohamed Abdillahi Ling'wenya

Shahidi: Urio: Mbona hujatuma majina na picha ya Adamoo ( Adamu Hassan Kasekwa, mshtakiwa wa pili?

Shahidi: Baadaye Urio apokea picha nyingine Kisha ujumbe usemao Adamu Hassan Kasekwa

Baada ya shahidi kumaliza kusoma ripoti hizo wakili Hilla anaomba ahirisho.

Jaji Tiganga anaahirisha kesi hiyo hadi saa 7:55 mchana huu ili upande wa mashtaka uendelee kumuongoza shahidi wake kutoa ushahidi wake.

Mahakama imerejea kwaajili Shahdi kuendelea kuhojiwa na wakili wwa serikali Piusi Hilla.

Shahidi: Baada ya kumaliza kufanya uchunguzi vielelezo hivi nilivifunga na kufihifadhi sikuviona tena hadi jana Ijumaa Januari 17.

Shahidi: Ijumaa iliyopita nilipigiwa simu na Inspekta Swilla kutakiwa kuja kutoa ushahidi kuhusiana na uchunguzi niliofanya.

Shahidi: Nilienda kuangalia kwenye register ya maabara ili kufahamu na Jumatatu tuliwasiliana aliniletea vielelezo.

Shahidi: Vielelezo hivyo ni simu nane na kwakuwa nilizifanyia kazi kwa kuangalia stika zilizokuwa kwenye simu zile…..

Shahidi: Hali ya vielelezo hivyo niliona jina langu na juu ya bahasha ilikuwa imeandikwa kwa makapeni.

Shahidi: Nilivihifadhi kwenye begi langu kwaajili ya usalama na kuja navyo mahakamani kwa ajili ya kuvitolea ushahidi.

Shahidi: Lakini jana kutokana na changamoto ya kiafya, nilirudi navyo na kwenda kuvihifadhi ofisini Kitengo cha uchunguzi wa kisayansi katika makao Makuu ya Polisi ya zamani na leo kuvichukua kuja navyo mahakamani.

Shahidi: Vielelezo hivyo vitakuwa na alama A, B, C, D, E, F, G na H ambapo kuna tekno nne Itel na Samsung ambazo zimeandikwa stika ya kijani.

Shahidi: Hivi ni vile vielelezo nilivyovifanyia kazi ni simu, kwenye hicho kimfuko kuna majina yangu, tarehe 9/7, 2020 lakini pia kuna kumbukumbu za maabara zimeandikwa kwa mkono.

 Shahidi: Mheshimiwa taarifa niliyowasiliaha awali ndio nilipoifanyia kazi naomba Mahaka yako izipokee kama kielelezo

Wakili wa utetezi baada ya kupitia vielelezo hivyo hawana pingamizi hivyo mahakama imepokea vielezo hivyo ambavyo ni simu nane kama kielelezo namba 28 hadi 35.

Wakili wa Serikali Piusi Hilla Mheshimiwa Jaji sina tena swali kwa shahidi.

Wakili wa utetezi Nashon Nkungu.

Wakili: Sahihi nisikia una miaka 37

Shahidi: Sahihi

Wakili: Kwani jeshi la Polisi unastaafu ukiwa na miaka mingapi

Shahidi: Sifahamu

Wakili: Ijumaa tarehe 14 tuliambiwa kuna Shahidi ni mstaafu anamuunguza baba yake

Shahidi: Sio sahihi

Wakili: Inawezekana wewee ndio ulityetoa hizi taarifa

Sahahid: Sio sahihi

Wakili: Ni sahihi ni kusema sio hacker anaweza kuingilia taarifa za mtu mwingine?

Shahidi: Sio kweli

Wakili: Hacker hawezi kuingilia na kudukua taarifa kwenye software

Shahidi: Sio sahihi

Wakili: Inawezekana kifaa kinachorun software kuingiliwa?

Shahidi: Haliwezekani

Wakili: Mwambie Jaji ulitumia muda gani kuchunguza vifaa vyako

Shahidi: Siku kadhaa

Wakili: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji ukikaa na hizo data zako kwenye kompyuta kwa muda gani

Shahidi: Sikumwambia

Wakili: Ulimwambia ni watu wangapi wana access na hicho chumba

Shahidi: Nilimwambia

Wakili: Pamoja na access mtu anaweza kuingilia

Shahidi: Ndio

Wakili: Baada ya kupokea majibu Julai,2, 2021 ndio ukaanza kufanyia uchunguzi

Shahidi: Hapana sikusema hivyo

Wakili: Ni sahihi toka tarehe 13,8,2020 ukaviweka na kuifanyia kazi tarehe 1/7/2021

Shahidi: So kweli

Wakili: Kutokana na ushahidi wako hakuna ukichokifanya hapao katikati

Shahaidi: Nilianza kuomba taarifa

Advertisement