Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shamte: Kujiuzulu Simai kuna kitu nyuma ya pazia

Muktasari:

  • Mohamed Shamte amesema suala la kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Muhammed Said, linafanya watu wajiulize mara 10.

Dar es Salaam. Kada wa zamani wa CCM, Mohamed Shamte amedai kuwa suala la kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Simai Muhammed Said lina kitu ambacho hakitajwi.

Mwanasiasa huyo aliyefukuzwa uanachama wa CCM mwaka 2022 kwa madai ya kutomheshimu Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameonya endapo kitu hicho kitafichwafichwa, wapo mawaziri wengine pia watajiuzulu.

Katika taarifa yake ya kujiuzulu iliyotumwa kwa njia ya video iliyotumwa mitandaoni, usiku wa kuamkia leo, bila kufafanua Simai amesema ni kutokana na imani yake kwamba jukumu la wasaidizi wa Rais, wakiwemo mawaziri ni kumsaidia katika kutekeleza ilani ya chama (CCM).

Akizungumza leo Januari 26 kupitia video iliyotumwa mitandaoni, Shamte amesema kujiuzulu kwa Simai ni sehemu ya demokrasia ya vyama vingi.

“Unaweza kujiuzulu kwa sababu unazo zimekukera inabidi uache au ukaona nimechoka kufanya hii kazi ya uwaziri, ukaamua kujiuzulu, lakini lazima there’s something behind (kuna kitu nyuma ya pazia).

“Kuna kitu na kwamba kujidai kufichaficha, haitakuwa waziri mmoja kufanya vile, kwa sababu naamini rohoni mwangu, wapo wanaoamini kufanya hivyo, wana hofu na wasiwasi,” amesema Shamte.

Amesema kujiuzulu kwa Simai kumemshtua, “nimejiuliza, jinsi alivyo Simai na namna alivyo close (karibu) na mteule wake, ni kitu ambacho kutokea kwake lazima wajiulize mara 10.”

Ameongeza kuwa, kujiuzulu huko kunatokana na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, tofauti na mfumo wa chama kimoja uliokuwepo.  

“Tulikuwa chama kimoja hapa, haya yote yasingetokea, ilikuwa ni kitu kizuri sana, tunachaguana bila zogo, bila tatizo, bila makundi, lakini sasa mfumo wa demokrasia ulipokuja mwaka 1992 ndio tumefika hapa sasa.

“Nyerere anasemaje, maendeleo sio vitu, maendeleo ni watu, wapate maendeleo ya shibe, makaazi mazuri, wavae vizuri, wale vizuri, washibe hawana njaa. Leo mapembe (mchele) Sh3, 000 (kwa kilo) maendeleo mazuri yanapatikana?” amehoji.

Taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari ikiwa imesainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said leo Januari 26, 2024, imeekeza kuwa Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameridhia kujiuzulu kwa Simai.

“Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini kifungu 129 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi amekubali ombi la kujiuzulu Mh. Simai Mohamed Said, Waziri wa Mambo ya kale kuazia Januari 26, 2024,” imesema.