Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Shirima wa Precision Air afariki, Profesa Mkenda amlilia

Marehemu  Michael Ngaleku Shirima

Muktasari:

  • Mbunge wa Rombo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda ameeleza kusikitishwa na  kifo cha mmiliki wa shirika la ndege la Precision Air, Mzee Michael Shirima na kusema kwamba  ameacha mambo mengi ya kujifunza.

Moshi. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda ameonesha kusikitishwa na  kifo cha mmiliki wa shirika la ndege la Precision Air, Mzee Michael Ngaleku Shirima na kusema kwamba  ameacha mambo mengi ya kujifunza.

Profesa Mkenda ambaye pia ni Mbunge wa Rombo na amesema Mzee Shirima ni mtu ambaye amefanya mambo makubwa katika nchi hii na kwamba yapo mambo mengi ya kuigwa kutoka kwake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 10 na shirika la ndege la Precision Air imesema Mzee Shirima amefariki saa tatu usiku Juni 9 katika hospitali ya Agha Khan mkoani Dar es salaam  alikokuwa amelezwa tangu Juni 8 mwaka huu akipatiwa matibabu.

Hata hivyo, leo alfajiri katika mitandao ya kijamii zilisambaa taarifa za kifo cha mzee Shirima huku baadhi wakionesha kusikitishwa na taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo maarufu hapa nchini.

"Taarifa za kifo za Mzee Shirima, zimenisikitisha  mno na nimeumia sana kwa kuondokewa na mzee wetu, hatuwezi kubadilisha au kufanya chochote, lakini maisha yake tuyatumie kama somo zuri sana kwa vijana na watu wote kwa bidii zake za kazi," amesema Profesa Mkenda

"Mzee Shirima ni mtu aliyefanya makubwa katika nchi hii na kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwake, ukisoma historia yake na bahati nzuri hivi majuzi tuu kaandika kitabu na kimezinduliwa, kinachoitwa "On my father's wings" utajifunza mambo mengi kuhusu maisha yake na kwamba alikuwa ni mtu wa aina gani,"

Profesa Mkenda amesema Mzee Shirima amekuwa ni mpambanaji wa kihistoria na hata alipoacha kazi shirika la ndege la Air Tanzania alifanya biashara ya kuchoma nyama, baadaye aliendesha malori kwenda Mwanza na alipambana mpaka alipoanzisha shirika hilo la ndege.

"Michael Shirima alikuwa akifanya kazi shirika la ndege la Air Tanzania, alivyoona uongozi hauendi vizuri wakati ule alijiuzulu kazi mapema sana akiwa na umri mdogo.

“Baada ya kutoka hapo alifanya kazi ya kuchoma nyama, akaanza kuendesha malori kwenda Mwanza akapambana mpaka baadaye akafika mahali akaweza kuendesha shirika la ndege la mtu binafsi ambayo ni kati ya mashirika makubwa sana hapa Afrika," alisema.

Amesema mzee huyo ni mfano wa kuigwa Afrika nzima, kutokana na tabia yake ya upole na uungwana.

Amesema maisha yake ni mfano mzuri wa kuigwa kwani alikuwa ni mtu wa kujitolea katika jamii na kwamba katika Wilaya ya Rombo ambako ndiko alipozaliwa amefanya mambo makubwa ikiwemo kuanzisha kituo cha watoto yatima na hivi karibu alikuwa anajenga Zahanati kwa ajili ya watoto yatima.