Songwe yaja na mambo nane kuziba mianya ya rushwa

Wadau wa vipimo wamefikia maazimio nane ambayo yatasaidia kudhibiti mianya ya rushwa katika mkoa wa Songwe ikiwemo kuendelea kutoa elimu zaidi kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusiana na kutumia huduma za wakala wa vipimo katika biashara zao.

Pia, wameazimia kuongeza juhudi katika kuwafikia wafanyabiashara wanaokaidi kuwasilisha mizani zao kwaajili ya ukaguzi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu zilizowekwa.

Maazimio hayo yamepitishwa katika warsha iliyofanyika jana jumatano, 5 Octoba, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi.

Warsha hiyo iliyowakutanisha wadau mbalimbali waliokua wanatoa matokeo ya uchambuzi wa mfumo ili kubaini mianya ya rushwa kwenye utendaji wa Wakala wa Vipimo (WMA) katika mkoa wa Songwe.

Akitoa matokeo ya utafiti huo, Naibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Songwe, Mohamed Shariff alisemakuwa lengo la taasisi hiyo ni kuimarisha utawala bora, kuzuia rushwa na kuchunguza rushwa katika taasisi mbalimbali.

Mohamed alisema katika utafiti huwa walibaini wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa matumizi ya huduma ya WMA kuhusiana na tozo zinazo tolewa na wakala huyo.

‘’Endapo wafanyabiashara wangepata elimu yakutosha na wakawa wanalipa tozo mbalimbali zinazolipwa kwa wakala wa vipimo serikali ingekusanya mapato ya kutosha kutokana na tozo au ada ambazo zingekusanywa kupitia huduma hizo.’’ alisema Mohamed.

Akisoma maazimio mengine, Ofisa kutoka TAKUKURU mkoa wa Songwe dawati la uzuiaji rushwa, Boniface Mwampashi walibaini kuwa  wafanyabiashara wafafanuliwe kwa uwazi juu ya tozo wanazopaswa kulipia kwaajili ya ukaguzi na matengenezo ya mizani zao na serikali kuiwezesha ofisi ya WMA mkoa wa Songwe wataalamu wakutosha pamoja na vitendea kazi vya kisasa ili kupanua wigo wa kukusanya mapato.

‘’WMA mkoa wa Songwe kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali  kupanua zaidi maeneo ya kukusanya mapato na TAKUKURU kwakushirikiana na wadau mbalimbali kufuatilia kwa ukaribu utendaji wa WMA katika mkoa wa Songwe ili iweze kuwa na utendaji wenye tija unaolenga kuboresha ukusanyaji wa mapato ya serikali wenye tija.’’ Alisema Mwampashi.

Sanjari na hayo maazimio mengine waliofikia ni pamoja na kuwa na umoja kutokuwa wakaidi katika matumizi ya mizani na wakala wa vipimo kuwa na ukaribu na maafisa mbalimbali wa serikali wanaowafikia moja kwa moja wananchi ikiwemo maendeleo ya jamii.

Akichangia katika warsha hiyo Meneja wakala wa vipimo mkoa wa Songwe, Robert Makule amewataka wafanyashara waachane na biashara za mazoea dunia ya sasa imebadilika.

‘’Warsha hii imekuwa yamafanikiko makubwa baada ya TAKUKURU kufanya utafiti na kugundua kuwa wafanyabiashara hawana elimu juu ya vipimo, wigo wa mapato na aina ya tozo kwaajili ya kuingiza mapato kwa serikali.’’  Alisema Robert.

Kwa upande wake Ofisa Mfawidhi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) mkoa wa Songwe, Ramadhani Omary amewapongeza TAKUKURU kwa uchambuzi nakushauri kuwa mizani zianzekukaguliwa kuanzia madukani zinapouzwa.