Tamasha la Sauti za Busara kuanza leo

Friday February 12 2021
sauti za busara pic
By Mwandishi Wetu

Zanzibar. Tamasha la 18 la Sauti za Busara linaanza leo Ijumaa Februari 12, 2021 eneo la mji Mkongwe mjini Unguja, Zanzibar huku vikundi 14 vikitarajiwa kutumbuiza vikiwemo 11 kutoka Tanzania.

Tamasha la mwaka 2021 linahusisha wasanii wengi watakaokuwa wanashiriki kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa mkurugenzi  wa Sauti za Busara,  Yusuf Mahmoud kuna mengi  ya kutarajia kutoka kwa wasani waliochaguliwa ambao watatangaza ubora wa Tanzania.

"Kwa miaka mingi watazamaji wamekuwa wakitarajia kitu cha pekee na kipya kutoka kwa timu yetu ya uteuzi na ndio sababu tunaamini safu ya mwaka huu ni bora, kwani ni ya Kiafrika kweli na ni kama tulivyokuwa tukisema muziki wenye kitambulisho,” amesema.

“Mchakato wa uteuzi wa wasanii umezingatia vizuizi vya kusafiri vinavyowekwa na nchi tofauti na kutokana na hali hiyo idadi kubwa ya vikundi mwaka huu ni kutoka Tanzania.”

Wasanii waliochaguliwa kushiriki ni Dulla Makabila, Msafiri Zawose, TaraJazz, Siti Muharam na Vitali Maembe wanawakilisha wasanii wa Tanzania.

Advertisement

Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani amesema Sauti za Busara inaitangaza Zanzibar na Tanzania na kuvutia wanamuziki wa kimataifa na kutoa fursa kwa wanamuziki kuonyesha kazi zao.

Advertisement