Tanesco waanza utekelezaji mradi wa umeme Ludewa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Wataalamu wa Tanesco watua Ludewa kutathimini ya mradi wa umeme unaozalishwa na kampuni ya Madope.

Ludewa. Wataalamu wa umeme kutoka Tanesco makao makuu wamewasili Ludewa kuufanyia tathimini mradi wa umeme unaozalishwa na kampuni ya Madope ili marekebisho yaanze kufanyika.

Hatua hii imefika baada ya Waziri wa Nishati, January Makamba wakati wa mkutano wa hadhara viwanja vya Shule ya Msingi Lugarawa kuwahakikishia wanabchi utekelezwaji wa mradi huo ili kuwapatia huduma wananchi.

Makamba alisema Serikali ipo tayari kununua umeme wote unaozalishwa na kampuni hiyo kuitaka kutuma barua ili atume wataalamu.

Mradi huu wa umeme ulikuwa unategemewa kuhudumia vijiji 20 ndani ya wilaya hiyo.