Tari kutoa mafunzo ya kilimo cha chikichi Kigoma

Tari kutoa mafunzo ya kilimo cha chikichi Kigoma

Muktasari:

  • Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari)mkoani Kigoma inatarajia kutoa elimu ya  kilimo bora cha mbegu mpya za michikichi aina ya Tenera.

Kigoma. Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari)mkoani Kigoma inatarajia kutoa elimu ya  kilimo bora cha mbegu mpya za michikichi aina ya Tenera.

Akizungumza leo Jumatano Oktoba 6, 2021, wakati akitoa elimu kwa wakulima wa zao hilo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkurugenzi wa Tari wa kituo cha Kihinga, Dk Filson Kagimbo amesema awamu ya kwanza ya mafunzo wameshatoa kwa wilaya za Kibondo, Uvinza, Kakonko na Manispaa ya Kigoma Ujiji na baadaye watamalizia wilaya ya Kigoma, Buhigwe na Kasulu.

Amesema mbegu mapya ya tenera inauwezo wa kuzalisha tani za mafuta 4 hadi 5 kwa hekta huku mbegu ya zamani ya dura ikizalisha tani 1.6 kwa hekta.