Tarura kutekeleza miradi yenye thamani ya bilioni 621

Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seif

Muktasari:

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) katika mwaka wa bajeti 2022/2023 umepanga kutekeleza jumla ya zabuni 1706 zenye thamani ya Sh 621.66 bilioni.

Dodoma. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura) katika mwaka wa bajeti 2022/2023 umepanga kutekeleza jumla ya zabuni 1,706 zenye thamani ya Sh621.66 bilioni.

  Hayo yamesema leo Jumatatu Oktoba 3, 2022 na Mtendaji Mkuu wa Tarura, Victor Seif wakati akizungumzia utekelezaji wa shughuli za Tarura na mwelekeo wa utekelezaji wa mwaka 2022/2023.

“Awamu ya kwanza tulitangaza asilimia 60 ya bajeti sawa na zabuni 1,085 zenye thamani ya Sh378.56 bilioni lengo likiwa ni kuanza mapema kabla ya msimu wa mvua kuanza,”amesema.

Amesema wameanza utekelezaji wa awamu ya pili ya asilimia 40 iliyobaki na kwamba zabuni 1,700 ambazo zina gharama ya zaidi ya Sh3 bilioni zinatangazwa katika kwenye ngazi ya Tarura ya mikoa.

Mtendaji mkuu huyo amesema zabuni sita ambazo gharama yake ni zaidi ya Sh3 bilioni zinatangazwa katika ngazi ya Tarura.

Aidha, amesema mradi wa ujenzi wa daraja na uendelezaji wa Bonde la Mto Msimbazi ni Dola za Marekani milioni 260 uko katika hatua ya maandalizi.