TBS yateketeza bidhaa hafifu yakiwemo maziwa ya watoto

TBS yateketeza bidhaa feki yakiwemo maziwa ya watoto

Muktasari:

  • Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imekamata vyakula vilivyoisha muda wake ikiwemo maziwa ya watoto na vipodozi vyenye viambata sumu visivyoruhusiwa nchini.

Mtwara. Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imekamata vyakula vilivyoisha muda wake ikiwemo maziwa ya watoto na vipodozi vyenye viambata sumu visivyoruhusiwa nchini.

 Bidhaa zilizoteketezwa ni pamoja na maziwa ya watoto wadogo, vinywaji na vipodozi i vyenye thamani ya Sh12.6 milioni.

Akizungumza mara baada ya kuteketeza bidhaa hizo Michael Mayala ambaye ni ofisa udhibiti ubora kutoka TBS amesema katika kamatakamata hiyo vipodozi vimeonekana kuwa vingi zaidi ya vyakula.

Amesema mbali na maziwa ya watoto wadogo, pia walikamata unga na mafuta ya kupikia, juisi na soda.

“Wafanyabiashara wanatakiwa kuingiza nchini bidhaa ambazo zinaruhusiwa zenye vibali vya TBS ili visiwe na madhara kwa wanaotumia pia kuna vyakula vilivyopitisha muda wake hivi ni hatari wananchi wanapaswa kuwa makini kuangalia muda wa matumizi kwa vyakula wanavyonunua madukani.”

“Tumekuta vipodozi vingi zaidi Mtwara Mjini, Newala, Masasi na Nanyumbu sio tu haviruhusiwi pia vina madhara kwa ngozi na afya kwa ujumla ndio maana  tunawataka wafanyabiashara wazingatie sheria za uingizwaji wa bidhaa nchini,” amesema Mayalla.