Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

THRDC: Ripoti ya CAG ni sehemu ndogo katika kuibua madudu

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),  Onesmo Ole Ngurumwa.

Muktasari:

  • Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) imeendesha mjadala wa Twitter Space ukiwa na mada ‘nini kinapaswa kufanyika ili ripoti za CAG ziwe na tija kwa Taifa? Na kushirikisha wadau mbalimbali.

Moshi. Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),  Onesmo Ole Ngurumwa amesema Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni sehemu ndogo sana katika kuibua maovu katika taasisi za umma.

Ngurumwa ameyasema hayo leo Jumatano, Aprili 12, 2023 wakati akichangia mjadala wa Twitter Space iliyoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) ukiwa na mada ‘nini kinapaswa kufanyika ili ripoti za CAG ziwe na tija kwa Taifa?

"Ofisi ya CAG ni sehemu ndogo sana na mimi sidhani kama kilicho gunduliwa na CAG ndio hali halisi, utakuta kuna mambo mengi sana pengine hata ofisi ya CAG isiyakute kwa sababu ni zoezi ambalo linafanywa mara moja kwa mwaka na ni taasisi zote za Kitaifa," amesema

Amesema ripoti iliyotolewa na Ofisi ya CAG pekee itakuwa haitendei haki Taifa kwa sababu matatizo ya nchi hii ya usimamizi wa rasiliamali za kitaifa ni makubwa na ni lazima mifumo mingine iangaliwe.

"Hatulitendei haki Taifa, kwa sababu matatizo ya nchi hii ya usimamizi wa rasilimali za kitaifa ni makubwa na ni lazima tuangalie mifumo mingine," amesema Ole Ngurumwa

Awali, Kaimu Mhariri wa Biashara na Uchumi wa Gazeti la Mwananchi, Ephrahim Bahemu amesema, kunahitaji kufanyiwa kazi mapendekezo ya CAG, mifumo na taratibu zilizowekwa zifuatwe katika taasisi wakati wote ili kuepuka madudu ambayo yamekuwa yakijitokeza.

Bahemu amesema,“…vyombo vya dola vya uchunguzi vinapaswa kuchukua hatua kwa wale wanaotajwa kwenye ripoti ya CAG.”

Mjadala huo unafanyika siku chache kupita tangu Ripoti za CAG Charles Kichere za mwaka wa fedha 2021/22 kuwasilishwa bungeni jijini Dodoma zikiwa zimeibua ubadhirifu kwenye maeneo mbalimbali.

Tayari Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza taasisi na mamlaka za Serikali kuzipitia ripoti hizo, kujibu na hatua zichukuliwe kwa watakaobainika.