TICTS yaendeleza rekodi yake ya utendaji kazi bora

Mpango wa uwekezaji unaoendelea wa TICTS ulishuhudia kuwasili cranes tatu za ziada za mpira mapema mwaka huu.

Muktasari:

Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) imevunja rekodi yake ya mwezi ya kuhudumia mizigo kwa mara nyingine tena.

Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) imevunja rekodi yake ya mwezi ya kuhudumia mizigo kwa mara nyingine tena.

Ikiwa imetoka kufanya vyema mwezi Machi kwa rekodi ya aina yake, imeshuhudiwa ndani ya mwezi Juni ikiweka rekodi ya kupokea mizigo ipatayo tani 61,450 kwa mwezi.

Kutokana na uchapakazi wa wafanyakazi wa TICTS, kituo pia kimeweza kushuhudia mabadiliko makubwa ndani ya mwezi huo. Juni 21, wafanyakazi waliweza kuhudumia zaidi ya tani 1000 za mizigo katika kipindi cha saa nane tu.

Katika muktadha mwingine, kituo kilifanikiwa kuhudumia magari yanayoingia na kutoka getini yapatayo 38,283 katika mwezi huo huo.

Akizungumzia mafanikio hayo, Matthew Clifft, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TICTS alisema, “Tunajivunia sana timu zetu zilizofikia rekodi hii mpya. Lengo letu kuu ni kurahisisha ufanyikaji wa biashara, kupunguza muda wa utoaji huduma.

Kwa kuzingatia hili, tunajitahidi kuhakikisha kwamba kituo chetu kinaweza kufikia viwango hivi vyenye tija kwa msingi endelevu.”

TICTS tayari imewekeza zaidi ya Sh12.5 bilioni katika vifaa mwaka huu na ina nia ya kusaidia serikali katika maono yake ya muda mrefu ya bandari ya Dar es Salaam.

TICTS ni mwanachama wa Hutchison Ports, bandari na huduma zinazohusiana na tawi la kampuni ya CK Hutchison Holdings Limited.

Ina mtandao wa vituo vya kuhudumia mizigo katika bandari 52 zinazojumuisha nchi 26 katika mabara ya Asia, Mashariki ya Kati, Afrika, Ulaya, Amerika na Australia.