Tozo Badari ya Lushamba Kanyala yapunguzwa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Hatimaye tozo iliyokuwa ikilalamikiwa na wananchi wanaotumia Bandari ya Lushamba Kanyala imeshushwa kutoka Sh600 hadi Sh400.

Buchosa. Hatimaye tozo iliyokuwa ikilalamikiwa na wananchi wanaotumia Bandari ya Lushamba Kanyala imeshushwa kutoka Sh600 hadi Sh400.

Kauli hiyo imetokewa na Meneja wa Mamlaka ya Bandari Kanda ya Ziwa, Vecent Stephano Novemba 26, 2021 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Kanyala wilayani Buchosa.

Awali kila mwananchi alikuwa anatozwa Sh600 akiingia na Sh600 anapotoka ambapo wananchi walilalamikia tozo hiyo kuwa kubwa.

Stephano amesema Serikali baada ya kusikia kilio cha wananchi juu ugumu wa maisha wa kushindwa kulipa tozo wanapotumia bandari hiyo tozo hiyo imepunzwa hadi Sh400.

"Suala la kupungaza tozo halikuwa dogo… hatimaye tozo hiyo imepungua kwenye maziwa yote yaliyoko hapa nchi" amesema Stephano.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo amesema haikuwa kazi rahisi jambo hili hadi kufanikiwa tunaishukuru Serikali Kwa kusikiliza kero ya wananchi.