TPSF yaishauri Serikali kuwekeza zaidi kwenye mazao ya kimkakati

Sunday June 13 2021
tija pic

Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Francis Nanai akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la alizeti unaofanyika mkoani Singida, leo. Kauli mbio ya mkutano huu ni zalisha alizeti kwa uhakika wa mafuta ya kula, kipato na maendeleo ya viwanda. Picha na Edwin Mjwahuzi

By Noor Shija

Singida. Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Francis Nanai ameishauri Serikali kuwekeza kwenye mazao ya kimkakati ili kuwa na kilimo chenye tija.

 Nanai amesema hayo leo Juni 13 kwenye mkutano wa kampeni ya kitaifa ya kilimo cha alizeti nchini, akisema kuwekeza kwenye mazao ya kimkakati kutasaidia nchi kuwa na tija kwenye kilimo.

Nanai pia ameishauri Serikali kutafuta masoko ya kuuza mazao hayo ya kimkakati badala ya kuwachia wakuma pekee.

Pia, ameishauri Serikali kuhakikisha ardhi bora kwa kilimo inalindwa na kuwezesha wakulima kuitumia kikamilifu.

Amesema ili kilimo kiwe na tija  kuna umuhimu kwa Serikali kufanyia kazi masuala ya utafiti, umwagiliaji, ugani na ubunifu.

Nanai ameishukuri Serikali kwa ajili ya kutenga zaidi ya Sh31 kwa ajili ya kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Advertisement

Pia, amesema jitihada za Serikali za kutoa zaidi ya Sh50 katika masuala ya ujuzi kutasaidia wajuzi nchini kwa kuna tatizo la wajuzi.


Advertisement