TRC: Ajali iliyosababisha vifo na majeruhi ni hujuma

Muktasari:

  • Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea leo Jumatano Juni 21,2022 mjini Tabora na kusababisha vifo na majeruhi kimetajwa  kuwa ni hujuma.

Tabora.  Chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyotokea leo Jumatano Juni 21,2022 mjini Tabora na kusababisha vifo na majeruhi kimetajwa  kuwa ni hujuma.

Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini (TRC), Masanja Kadogosa amesema kuna kipande cha reli kiliondolewa na kisha kurudishwa kwa kuegeshwa ili kisionekane kama kimeegeshwa.

Kadogosa amebainisha kuwa mwendo wa treni hiyo ulikuwa mdogo na kama ungekuwa wa kasi kubwa basi madhara yangekuwa makubwa zaidi kwa vifo na majeruhi.

"Eneo lililopata ajali treni hiyo lipo  jirani na makazi ya watu na mara zote treni za abiria na mizigo huwa zinapita kwa mwendo wa pole," amesema.

Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Honoratha Rutatinisibwa amesema bado wanaendelea kuhesabu waliofariki na majeruhi wa ajali hiyo na

Honoratha hakutaka kujibu kama waliofariki ni wanne au watatu akibainisha kuwa wanaendelea kuhesabu ingawa mmoja wa watumishi wa hospitali ya Kitete aliyeomba kuhifadhiwa ya jina lake amesema waliofariki ni zaidi ya wanane.