Trump kuanzisha chama chake kipya

Thursday January 21 2021
trumppic

Rais wa Marekani aliyemaliza muda wake, Donald Trump

By Mwandishi Wetu

Marekani. Rais wa Marekani aliyemaliza muda wake, Donald Trump anakusudia kuunda chama kipya cha siasa kitakachoitwa Patriot Party, baada ya kuwaambia wafuasi wake katika hotuba yake ya kuliaga Taifa kwamba “harakati walizozinzisha ndiyo zinaanza.”

Rais huyo alisema anazungumza na wasaidizi wake juu ya wazo hilo, The Wall Street Journal liliripoti. Hata hivyo, haijajulikana ni kiasi gani anamaanisha katika kutekeleza wazo hilo.

Trump aliapa kuendelea kuwepo katika majukwaa ya kisiasa na kwamba “harakati” zake ndiyo kwanza zimeanza.

“Sasa ninapojiandaa kukabidhi madaraka kwa utawala mpya saa sita mchana, nataka ujue kuwa harakati tulizoanzisha ndiyo zimeanza,” alisema.

Hata hivyo, dhamira yake ya kutaka kuendelea na siasa kunaweza kusababisha hofu kwa wafuasi wengine wa Republican na kuzidi kuwagawa kama ilivyokuwa awali.

Advertisement