Uchaguzi wa wabunge, magavana waahiriswa

Muktasari:

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)  nchini Kenya imeahirisha uchaguzi wa gavana wa Mombasa na Kakamega pamoja wabunge wa Kacheliba na Pokot Kusini baada ya karatasi za kupigia kura kuonekana zina maelezo tofauti.

Kenya. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)  nchini Kenya imeahirisha uchaguzi wa gavana wa Mombasa na Kakamega pamoja wabunge wa Kacheliba na Pokot Kusini baada ya karatasi za kupigia kura kuonekana zina maelezo tofauti.

Uamuzi huo umetangazwa leo na Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati ambapo amesema watatangaza tarehe nyingine ya kufanya uchaguzi huo kupitia tangazo kwenye gazeti la Serikali.

Hata hivyo Chebukati hakuwa tayari kueleza kwa undani kasoro hizo zilizosababisha wachukue uamuzi huo.

Tangu asubuhi kumekuwa na madai kutoka kwa wagombea wa nafasi mbalimbali wa Kenya Kwanza kuwa kuna mienendo isiyofaa wanayohisi inafanywa kuwabeba wenzao wa Azimio la Umoja.

Licha ya changamoto hizo, Wafula ameahidi kuwa uchaguzi utafanyika kwa uhuru na haki hivyo Wakenya wasihofie chochote.