Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uelewa wa watu kujua haki zao waongezeka

Mbobezi wa haki za binadamu nchini, Dk Elifuraha Laltaika akizungumza na wanafunzi wa sheria katika chuo cha Makumira wakati wa maadhimisho ya siku ya haki za binadamu Afrika yaliyofanyika chuoni hapo.Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

  • Wadau wa haki za binadamu nchini wamesema jitihada zinazofanywa na baadhi ya vyuo vikuu kutoa kozi ya haki za binadamu imesaidia kwa kiasi kikubwa jamii kuzijua na kuzitambua haki zao




Kwa ufupi:



Janeth Joseph,Mwananchi [email protected]


Arusha. Wadau wa haki za binadamu nchini wamesema jitihada zinazofanywa na baadhi ya vyuo vikuu kutoa kozi ya haki za binadamu na msaada wa kisheria unaotolewa na Chama cha Mawikili Tanganyika (TLS) umesaidia kwa kiasi kikubwa jamii kuzijua na kuzitambua haki zao.

Hayo yamesemwa na mbobezi wa haki za binadamu nchini, Dk Elifuraha Laltaika wakati wa siku ya maadhimisho ya haki za binadamu kwa Afrika ambapo kwa Afrika yamefanyika katika chuo cha Makumira kilichopo Mkoani Arusha.

"Sasa hivi watu wanapenda kudai haki zao na hii ni ishara ya watu kujua haki zao na wanajua zinapatikana wapi na ukizingatia vyuo vyetu vikuu vinatoa kozi ya haki za binadamu,"amesema Dk Laltaika na kuongeza

"Katika siku maalumu kuna wiki za sheria ambapo nchi mbalimbali zinatoa msaada wa kisheria na hapa nchini chama cha mawakili Tanganyika kimekuwa mstari wa mbele na wakati mwingine kuwatetea bure kabisa ili wapate haki zao huko zinakopatikana,"

Akizungumzia umuhimu wa jamii kuzitambua haki zao, Rais wa chama cha wanasheria katika chuo cha Makumira, Ibrahim Ayubu amesema ipo haja ya jamii kuendelea kupaza sauti kwa ajili ya watu wanaonyimwa haki zao katika jamii hasa zile za maisha ya kawaida.

"Tunaamini pasipokuwa na haki za binadamu hakuna demokrasia, hakuna kitu jamii itakachoweza kufanya zaidi ya machafuko na mambo mengine ambayo kiuhalisia yatafupisha maendeleo yetu,"

"Siku haki za binadamu inatukumbusha Waafrika tusimame kwa umoja wetu tufanye  kazi zetu kwa uhuru na haki sawa kwa watu wote ili kuendelea kukumbuka mchango wa watu waliotoa katika kupeleka haki za watu mbalimbali na watu wakatambua haki zao.

Naye Ofisa kutoka mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu, Dk.Mwiza Nkhata  amesema  maadhimisho hayo yanasaidia kukumbusha watu umuhimu wa kuzijua na kuzitambua haki zao za msingi katika nyanja mbalimbali za kijamii