Ufaransa na Tanzania: Washirika wa ajenda ya uchumi wa bluu

Muktasari:

  • Uchumi wa bluu unamaanisha “matumizi endelevu ya rasilimali za bahari kwa ukuaji wa uchumi, maisha bora, na kazi huku ikolojia ya bahari ikihifadhiwa.”

Je! uchumi wa bluu unamaanisha nini kwa Tanzania na Zanzibar?

Uchumi wa bluu unamaan-isha “matumizi endelevu ya rasilimali za bahari kwa ukuaji wa uchumi, maisha bora, na kazi huku ikolojia ya bahari ikihifadhiwa.”

Tanzania ina rasilimali nyingi zinazohusiana na bahari: Ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa na Rukwa ambayo yanachangia asilimia 37 ya eneo lote la nchi; ukanda wa pwani wa kilo-mita 1,424 na mamia ya visiwa huko Zanzibar.

Ajenda ya uchumi wa Bluu imekuwa kipaumbele kikubwa kwa Tanzania bara na Zanzibar. Rais Samia Suluhu Hassan alifafanua uchumi wa Bluu kama kipaumbele katika hotuba yake ya kwanza kwa Taifa, wakati huo huo Rais Hussein Mwinyi aliunda Wizara maalumu ya uchumi bluu. Siyo tu juhudi hizi zitaifanya Tanzania kuendeleza matumizi endelevu ya rasilimali zake za baharini, maziwani na fukweni, lakini nchi inaweza kuwa kiongozi katika mkakati wa uchumi wa Bluu katika miaka michache ijayo.

Mkakati wa uchumi wa bluu wa Ufaransa katika Bahari ya Hindi

Kama wanachama wa Chama cha Ukanda wa Bahari ya Hindi (IORA), Ufaransa na Tanzania watashirikiana kwa karibu zaidi juu ya kipaumbele hiki cha pamoja. Kwa sababu ya kuwa na maeneo yake ya ng’ambo katika ukanda huo - Mayotte na La Réunion, visiwa maarufu zaidi vya Ufaransa - Ufaransa imekuwa mwanachama wa IORA mwaka 2020.

Chama hiki chenye nguvu kinachohusisha Serikali za nchi kadhaa kinakusudia kuimarisha ushirikiano na maendeleo endelevu ndani ya ukanda wa Bahari ya Hindi kupitia nchi wanachama 23 kwa kuzingatia usalama wa baharini; biashara na uwekezaji; utalii; mabadilishano ya kada za elimu, sayansi na teknolojia; udhibiti wa shughuli za uvuvi; hatari za majanga; uwezeshaji wanawake kiuchumi; na, mwishowe… uchumi bluu. Uchumi wa bluu pia ni kipaumbele cha uenyekiti wa Ufaransa wa Tume ya Bahari ya Hindi (IOC) kwa mwaka 2021/22. IOC imekuwa kwa zaidi ya miaka 30 sasa, Tume pekee ya Kiafrika ambayo Ufaransa ni mwanachama wake, pamoja na Comoro, Madagascar, Mauritius na Seychelles.

Katika mfumo wa urais wake wa IOC, Ufaransa itaongeza ushirikiano wake na eneo lote na Tanzania, katika nyanja kadhaa, pamoja na usalama katika eneo la bahari, uchumi wa kikanda, utunzaji wa mazingira na udhibiti wa hatari za kimazingira.

Je, Ufaransa inawezaje kusaidia mkakati wa uchu-mi wa bluu wa Tanzania?

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania tayari unasaidia miradi miwili inayohusiana na uchumi wa bluu. Mradi wa kwanza unatekelezwa na Kikundi cha Uhifadhi wa Misitu Tanzania (TFCG), kinachokuza elimu ya mazingira na ulinzi wa bayoanuwai katika misitu ya pwani. Mradi wa pili, unaitwa “Plastiki yako mazin-gira yetu” unatekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Nipe Fagio na unalenga uzalishaji na matumizi ya plastiki inayotumika mara moja nchini Tanzania, ikikuza utaratibu uhifadhi wa taka nchini. Kwa kuongezea, Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) linatekeleza na Tanzania, mkakati wake wa bahari, ikiongoza shughuli za kikundi katika maeneo ya baharini na pwani.

Kwa mfano, AFD inafadhili Mradi wa AquaCoco, unaohusishwa na juhudi za ufugaji samaki na uhifadhi ikitekeleza kwa ushirikiano na shirika la IUCN.

AFD pia inafanya kazi na Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ili kutekeleza mradi wa upandaji miti duniani.

Majadiliano juu ya mambo mengi ya uchumi wa bluu yanaendelea kati ya Ufaransa, Tanzania na Zanzibar ili kuchangia pamoja katika mkakati kabambe wa uchumi wa bluu, wenye manufaa kwa nchi zetu zote lakini pia kwa eneo lote la Bahari ya Hindi.