Uongozi wa wafanyabiashara Karume kukutana na RC Makalla leo

Wafanyabiashara wa soko la Karume lililoungua wakiwa wameandamana kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Picha na Tatu Mohamed

Muktasari:

  • Wakati wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) wakiendelea kuweka alama maeneo yao, uongozi wa wafanyabishara hao leo utakuta na kufanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla.

Dar es Salaam. Wakati wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) wakiendelea kuweka alama maeneo yao, uongozi wa wafanyabishara hao leo utakuta na kufanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla.

Hayo yamesemwa leo Januari 18, 2022 na msemaji wa wafanyabishara hao, Ismail Feisal wakati anazungumzia na Mwaanchi.

Amesema wamepewa taarifa ya kufanya kikao na kiongozi huyo pamoja na viongozi wa soko la Karume ambalo limeungua moto usiku wa kuamkia Jumapili.

Mabomu ya machozi yarindima Dar

"Tunajiandaa kuingia kwenye kikao kwenda kujua kinachoendelea na hakuna taarifa nyingine yeyote zaidi ya hicho kikao na Mkuu wa Mkoa japo hatujaambiwa muda wa kufanyika," amesema

"Hadi sasa hivi hakuna taarifa mbaya kwa upande wetu na shughuli za kuweka alama zinaendelea kama kawaida na watu wa uchunguzi wanaendelea na majukumu yao pamoja na maaskari," amesema

Amesema utulivu umetawala kwenye soko hilo wakati wafanyabishara wakiendelea kuweka alama kwenye maeneo yao huku wakisubiria ripoti ya kamati iliyoundwa na Serikali kwa ajili ya kuchunguza chanzo cha ajali hiyo pamoja na hasara iliyopatikana.