Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Upelelezi kesi ya uhujumu uchumi Moshi wakamilika

New Content Item (1)

Muktasari:

  • Upande wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi namba 5 ya mwaka 2023, iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi watatu wa benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) umeieleza Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Moshi. Kesi ya uhujumu uchumi ambayo inawakabili waliokuwa wafanyakazi watatu wa benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL), upelelezi wake umekamilika huku upande wa mashitaka ukiwasilisha mahakamani vielelezo 471 na mashahidi 29.

Kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2023 ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Salome Mshasha huku upande wa mashitaka ukiongozwa na Mawakili wa Serikali Donasian Chuwa, Samwel Kaaya, Henry Kasiano Daudi na Bora Msafiri Mfinanga.

Octoba 2019,  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa iliwafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, aliyekuwa Meneja Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo, Joseph  Kingazi, na aliyekuwa Meneja Mkuu wa benki, Elizabeth Makwabe, wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali ikiwemo uhujumu uchumi.

Hata hivyo, baadaye Juni, 2021 aliyekuwa mhasibu wa benki hiyo, aliunganishwa katika kesi hiyo.

Washitakiwa hao kwa pamoja walikuwa wanashtakiwa kwa makosa 13, yakiwemo makosa 9 ya kughushi na kutoa nyaraka za uongo, kosa moja la kuongoza uhalifu wa kupanga, kosa moja la ubadhirifu wa fedha za umma na kuisababisha hasara ya zaidi ya Sh2.4 bilioni.

Akisoma maelezo ya mashahidi (Commital proceedings) leo Jumanne, Julai 11, 2023, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Donasian Chuwa, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha ameielezea mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

"Katika usikilizwaji wa kesi hii ya uhujumu uchumi ambayo upelelezi wake umekamilika, upande wa mashtaka tukatakuwa na mashahidi 29 pamoja na vielelezo 471," Wakili Chuwa ameiambia mahakama hiyo.

Hata hivyo, baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha maelezo hayo, Hakimu Mshasha aliwaeleza washitakiwa hao kuwa, kwa kuwa mahakama imewafahamisha na kusikia idadi ya mashahidi pamoja na vielelzo vitakavyotumika wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo katika Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi, chochote watakachokisema mbele ya mahakama hiyo kitatumika kama ushahidi wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Hivyo washitakiwa hao kwa pamoja, walimweleza hakimu Mshasha kuwa watakuwa na mashahidi wao pamoja na vielelezo vyao.

Hakimu Mshasha aliwaleza washitakiwa hao kuwa wataendelea na dhamana yao mpaka hapo watakapopewa taarifa rasmi juu ya usikilizwaji wa kesi hiyo.