Ushindi wa kishindo uchaguzi nafasi ya mwenyekiti CCM Sengerema

Mwenyekiti mteule wa CCM wilaya ya Sengerema Marco Makoye (kushoto) akifurahi baada na wajumbe baada ya kutangazwa mashindi usiku huu.

Muktasari:

Wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema wamekubali matokea baada ya Marco Makoye kutanzwa kuwa mshindi wa nafasi hiyo.

Sengerema. Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa, Marco Makoye aliyekuwa akitetea nafasi yake, ameshinda tena baada ya kuwabwagwa wapinzani wake kwa kupata kura 1,178.

Mbali na Makoye wagombea wengine walikuwa pamoja na Chasama Kamata aliyepata kura 325 na Masele aliyepata kura 19 kwenye uchaguzi.

Kutokana na kura hizo msimamizi wa uchaguzi Lameck Mahewa ametangaza Marco Makoye kuwa Mwenyekiti mteule wa CCM wilaya ya Sengerema.

Katika matokeo hayo kura zilizopigwa 1525 kura 3 zimeharibika kura halali 1525.

Chasama ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa CCM mwaka 2007hadi 2012 amekubali matokeo na kuwashukuru wanaCCM.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo baadhi ya wajumbe wamepongeza hatua hiyo na kusema kuwa Marco Makoye alikuwa anastahili kupata kura hizo kutokana na utendajinkazi wake ndani ya CCM.

Akizungumza baada ya uchjaguzi huo, Chasama Kamata amewashukuru wanaCCM waliompigia kura na kusema ataendelea kuwa mwanachama mtiifu na ataendelea kushirikiana na viongozi waliochaguliwa ili kukidumisha chama.

Wajumbe waliochaguliwa kwenda mkutano mkuu Taifa wa CCM Joshua Shimiyu, Omari Sukari, sambamba na Jackini George.

Kwa upande wake Joshua Shimiyu baada ya kuchaguliwa amewaahidi wa Sengerema utumishi uliotukuka katika utumishi wake kwenye nafasi hiyo.

Maxmiliani mpuya mmoja wa wajumbe waliokuwa kwenye uchaguzi huo amesema maamuzi hayo yaliyofanywa na.wajumbe ni haki yao kikatiba.