Ushuru mabasi mradi wa mwendokasi yanayoingizwa Tanzania kupunguzwa

Thursday June 10 2021
ushurupic
By Fortune Francis

Dar es Salaam. Serikali imependekeza kupunguzwa kwa ushuru wa forodha kutoka asilimia 25 hadi 10 kwa mwaka mmoja kwa mabasi ya abiria yanayotambulika kwa HS Codes 8702.10.99 na 8702.20.99 yanayoingizwa nchini kwa ajili ya mradi wa mwendokasi.

Hatua hii inalenga kupunguza gharama za uingizaji wa mabasi hayo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi Juni 10, 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/22.

Amesema hatua hii inalenga kupunguza gharama za uingizaji wa mabasi hayo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi.

Pia, Serikali imependekeza kuongeza ushuru wa forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 kwa mwaka mmoja kwenye nyuzi za pamba  zinazotambulika kwa Headings 52.05, 52.06 na 52.07 lengo la hatua hii ni kulinda viwanda vinavyozalisha bidhaa hiyo na kuongeza thamani ya zao la pamba nchini.

Maeneo mengine waliyopendekeza kuongezeka kwa ushuru wa forodha kutoka asilimia 10 hadi asilimia 25 ni matairi mapya ya pikipiki yanayotambulika kwa HS Code 4011.40.00 ili  kuongea mapato ya Serikali kwa kuwa matairi haya ni bidhaa zilizokamilika kwa ajili ya mtumiaji.

Advertisement
Advertisement