VIDEO: CCM wakubali Katiba Mpya

Wednesday June 22 2022
ccmpiiic
By Mwandishi Wetu

Dodoma. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeiomba Serikali kuangalia namna bora ya kufufua na kukwamua mchakato wa Katiba mpya kwa maslahi mapana ya Taifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatano Juni 22,2022 Jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema katika kikao cha Kamati kuu ya Halmashauri Kuu walichokaa wamekubaliana suala la Katiba mpya liangaliwe kwa maslahi mapana ya Taifa.


Advertisement