VIDEO: Maalim Seif atembelea mradi daraja la Kigogo-Busisi

Thursday January 14 2021
By Mgongo Kaitira

Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ametembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2 litakalounganisha wilaya ya Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza.

Maalim Seif  ametembelea ujenzi huo leo Alhamisi Januari 14, 2021 wakati akielekea wilayani Chato Mkoa wa Geita. Mradi huo unagharimu Sh699 bilioni na unatarajiwa kukamilika 2024.

Advertisement